Akatazwa Kuachia Wimbo Na Mpenzi Wake
Ni msanii ambaye ana potential ya kuja kua msanii mkubwa
sana wa hophop kutoka Pwani. Flamez
ambaye alikua amejipanga kuachia track yake mpya ya PENZI LA ATM aliyomshirikisha Shaa
Biggy imebidi asitishe project hio kisa
mapenzi.
Kilichoimbwa katika wimbo huo ndio sababu kubwa iliyofanya
kutokea kwa mtafaruku huo wa kusababisha track hio kufikia kusitishwa. Katika
track hio, Flamez anasuta mabinti
ambayo wameendekeza pesa mbele katika mapenzi na mpenzi wake akaichukulia
akaona ya kwamba ujumbe huo umemlenga yeye.
‘Si kweli kwamba
nimelenga track hio kwa mpenzi wangu ila nilikua nimeongelea uhalisia wa vitu vinavyotokea
ila sasa yeye kaichukulia personal hadi kusema ya kwamba atajitoa katika
mahusiano yetu iwapo nitaachia track hio kwa kua anadhani ntakua namdhalilisha.’
Flamez amesema.
Flamez ambaye
vilevile alikua ashaanza mikakati ya kuaanda video ya track hio imembidi arudi
kwenye ‘drawingboard’ huku akisema ya
kwamba inamuuma sana ila hio baadhi ya changamoto ambazo wasanii wengi
wanapitia wakati wana,date watu wasioelewa kazi zao.
Comments
Post a Comment