Bizzy Kay Aanzisha Kampuni Ya Ku,manage Wasanii
KIMWANA, track
ambayo aliwashirikisha Ali B na Susumila ni moja kati ya track zake mbazo zimewahi kupendwa sana na
mashabiki. Bizzy K ambaye ana uwezo
mkubwa sana wa utunzi na kuimba katika siku za hivi karibuni ameonekana
kupunguza kasi yake ya mziki.
‘kwa sasa kidogo
nimepunguza kazi zangu za mziki, ila hivi karibuni naachia ngoma mpya. Kando na
usanii mimi ni mwanabiashara na sanasana nimeekeza katika ‘real estate’ hivyo
basi katika kufuatilia fuatilia hii mijengo yangu hua nashikika sana hadi
nakosa mda wa kufanya mziki. Lakini napenda mziki sana na mziki ni biashara
ambayo mtu akiifanya kwa ustadi itampa faida kubwa sana so nimeamua sasa nianze
ku,manage wasanii. Japo sitakua nawasimamia mimi mwenyewe moja kwa moja
kwasababu nitakua na manager na watu wengine watakaokua wanashuhulikia maswala
hayo, mimi ndiye nitakaye kua nasukuma mchakato mazima wa management hio’ Bizzy Kay amesema.
Akifafanua zaidi Bizzy
K amesema ya kwamba bado hajachagua wasanii ambao atakua anawa,manage lakini
analenga kua na wasanii watatu ambao tayari washainukia na watatu wanaochipuka.
‘Nitaweka kila kitu
wazi baada ya miezi miwili hivi, jina la kampuni hio, wasanii nitakao kua
nimewa,sign na managers wangu” Bizzy Kay amemalizia
Comments
Post a Comment