Susumila Rebrands ( video)
Amekua akijitangaza sana kupitia label yake ya MisheMishe
Music Empire na Rihaha Enterprises tangu 2014. Amepata mafanikio makubwa na
kupiga hatua kubwa toka nyakati hizo si kwa kuachia audio kali tu bali hata kufanya video zenye
ubora na viwango.
Wiki hii ikianza kupitia mtandao wa facebk, Susumila
ametanganza ya kwamba mwezi wa Agosti, tarehe 8 atakua anaachia wimbo mpya,
video mpya na label mpya akieleza ya kwamba ndio itakua MWANZO MPYA kwake.
Siku ya jumanne, 12 Julai, katika mahojiano ya simu na Lucas de Mackinon katika
kipindi cha MashavMashav University cha Pwani Fm, Susumila alieleza ya kwamba anakuja
kivingine na katika ujio huo wake na management atakua na team ambayo itakua na
dancers, cameraman, warembeshaji, mtaalam wa mawasiliano na mitandao ya
kijamii.
Comments
Post a Comment