Waathiriwa Wa Baa La Njaa Ganze Waanza Kupokea Msaada (picha)
Wiki jana eneo la Jila,
Bamba katika kaunti ya Kilifi
liligonga vichwa vya habari baada ya
kuangaziwa jinsi watu wanavyoteseka na njaa.
Zilikua habari za kushtusha na kuhuzunisha kwani watoto wanailisemekana
kwamba wapo ambao wamepoteza maisha kwa kukosa chakula madai ambayo serikali
imeyakana kwa kusema ni kweli kwamba watu wanatesekan na njaa ila hakuna
aliyepoteza uhai.
Habari hizo ziligusa wengi na kati ya walioguswa na habari
hizo ni Hasheem Omar (Rihaha)
ambaye anatokea kunti hio ya Kilifi.
Alimuomba director, Kalpesh Patel wa
kampuni anayoifanyia kazi (Export
Trading Co. Ltd) aingilie kati na kupitia kampuni hio wakapanga kuenda
kusaidia wa balaa la njaa huko Bamba.
Wakiwa na dozen 100
za vitabu, mbaazi tonne 10, maharagwe tani 6, unga wa mahindi tani 20, biskuti
catoni 100 na peremende katoni 8…ikiwa ni mzigo wa takriban Shilingi Milioni Mbili walifunga safari
hapo siku ya jumamosi kutoka Mombasa hadi
Kilifi ambapo waliambatana na county
Commissioner, deputy county commissioner wa kilifi na MCA wa Bamba hadi eneo la
Bandari ambapo ndio ilikua kituo cha
kwanza walipoganyiza chakula alafu baadae msafara huo ukaelekea hadi Jila ambapo ndio ilikua kituo cha pili
na cha mwisho kilichoweza kuganyiwa chakula. Kwa ujumla msaada huo uliweza
kufikia takriban familia 3000.
Akihutubia Wanahabari walioku wameambatana na msafara
huo,county commissioner alisema ya kwamba serikali ya kaunti na serikali ya
taifa zinashirikiana kukabiliana na baa hilo la njaa na wiki hii serikali ya
taifa itatuma magunia 1050 ya mchele, magunia
1050 ya maharagwe, katooni 350 za mafuta
ya kupikia. Chakula hicho kinatarajiwa kugawiwa katika subcounty zote za
kilifi.
Hizi hapa ni picha za tukio hilo lilolofanyika siku ya
jumamosi kwa niaba ya Export Trading
Company Limited…
Comments
Post a Comment