Wasanii Kutoka Likoni Wapewa kshs.500,000




Hapo jana  siku ya jumapili, 24-Julai Muwakilishi wa Wanawake wa kaunti ya Mombasa, Mishi Mboko aliweza kukabidhi wasanii kutoka Likoni, Talent House  hundi ya Kshs. 500,000.
Hundi hio ilitolewa wakati mheshimiwa Mishi Mboko alipokua akikabidhi mitaji/capital kwa makundi mbalimbali kutoka eneo la Likoni ili waanzishe mirandi itakayowapa uwezo wa kujitegemea na kujiendeleza kimaisha.

Fisherman ambao ni mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo la wasanii, Talent House kutoka Likoni ameeleza ya kwamba hundi hio wameweza kukabidhiwa baada ya kuandika proposal takriban miezi mitano iliyopita na kuiwasilishwa katika ofisi za muwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Mombasa.
‘…Haikua mara yetu ya kwanza kuwasilisha proposal kwani tuliwahi kuwasilishwa proposal katika afisi ya mbunge wa Likoni, mheshimwa Mwahima na afisi mbalimbali lakini hazikuwahi kupitishwa. Ni vigumu kupata usaidi haswa kifedha kutoka kwa waheshimiwa unless uwe na proposal lakini bila hivyo hawawezi kukupa pesa tu hivihivi’ Fisherman amesema.

Fisherman ambaye pamoja na Fat S na Producer Noor Mwamba waliubda kundi la Talent House ambalo ni kundi la wasanii zaidi ya 50 kama vile Dully Melody,  Yakuza Band, C New, Rudeboyz, Fungo Group…..kutoka Likoni ikiwa nia yao ni kuangalia jinsi ya kusaidika kwa kuja na mradi wa pamoja utakao wasaidia hao na wasanii wengine pia.
‘Tutatumia pesa hizi kununua vifaa vya kisasa vya studio ili kuhakikisha ya kwamba tunafanya mziki wenye quality ya juu ambayo ina hadhi na kuwasilishika. Tatizo kubwa limekua ni  wasanii  kusumbuka na quality ya mziki kwani vifaa vya kisasa ni ghali mno  ila sasa msanii atashindwa tu mwenyewe”  Fisherman ameeleza huku akiendelea kusema ya kwamba wasanii hawatakua wakirekodi bure kwani vifaa hivyo vitahitaji marekebisho na pia inafaa kua kama biashara kwa sababu hata yale makundi mengine yaliyokabidhiwa mtaji  kama vile masufuria bado watakua wanakodisha vifaa hivyo ili kupata kipato.

‘haitakua bure kurekodi katika studio hio itakayogaramiwa na pesa hizo ila kutakua na afueni kubwa kwani ada zake zitakua chini kabisa angalau producer alipwe na mahitaji ya kuendesha studio yaweze kutimizwa” Fisherman amemalizia.

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele