Beef Za Wasanii Wa HipHop Zilivunja Collabo Yao, Nyota Ndogo Na Afande Selle

Msanii Nyota Ndogo ambaye kwa sasa anatamba na kibao cha Subira Yangu amesisitiza matamanio yake ya hapo awali ya kutaka kuwaleta pamoja wasanii wote wa hip hop na kuwashirikisha katika track moja. Katika siku za nyuma, Nyota aliwahi kuandika orodha ya wasanii wa HipHop kutoka Mombasa ambao angependa kuwashirikisha na kufikia kiwango cha hadi kuahidi kumjumuisha Afande Selle kwenye ngoma hiyo.
Hata hivyo wazo hilo lilionekana kufifia huku mashabiki wakiachwa kwenye giza kuhusu haswa kilichosababisha kufeli kwa mradi huo. Leo hii Nyota ameweka wazi kilichosababisha kutofanyika kwa mradi huo alioupendekeza huku akisema alijaribu kivyovyote kuwafuata wasanii hao kuwasihi ila ikashindikana...
'Wasanii wa hiphop wanapenda saana kurushiana maneno hadi unashindwa utawa approach vipi,wale watu niliokua nimewachagua ambao nawaaminia hadi kuna mmoja nilimtaja jina niligundua kuwa wana chuki,sijui kama ni ya kutengeneza au ni ya ukweli lakini imeshindikana maana nakumbuka kuna mmoja nilimfuata na akasema mimi mama Nyota ukinieka na hao wengine mimi nitawatandika.'' Nyota amewahimiza wasanii wa Hip Hop kuweka tofauti zao kando ili kuendeleza mziki wao.  
''Napenda saana kuskiza mziki wa Hip Hop kwanza maandishi yao na mashairi wametushinda sisi waimbaji'' 
Msikilize Nyota Ndogo Akifunguka [[ HAPA ]]
NB; VibeCity Awards Mombasa zitafanyika hivi karibuni, na washabiki wanaoshiriki kupiga kura wanapata fursa ya kushinda airtime kati ya kshs.100 na kshs.1000. Washindi 10 kila siku kwa kupiga kura [HAPA]

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele