Kaa La Moto Na Archy Kawere Waanzisha TKP (Toa Kitambi Project)
Ni mmoja kati ya wasanii wakali wa Swahili hiphop hapa
nchini. Uwezo wake wa kuchana kwa lugha ya Kiswahili umeweza kumfanya
kupeperusha bendera ya hiphop hapa pwani. Kando na mziki, Kaa
La Moto anajivunia kuwa katika timu ya taifa ya mchezo wa Karate. Aliposhirikiana na Sis P katika video yao ya wimbo ITS OK, alimsaidia pakubwa msanii huyo
wa kike kufanya mazoezi ili kuwa na mwili wenye muonekano mzuri katika video
hio.
Vilevile amekua na ukaribu na Archy Kawere ambaye ni mke wa msanii mkongwe wa hiphop hapa pwani, Johnny Skani ambaye ni mmoja wa wahusika wa kipindi
ambacho kimezua gumzo hata kabla kuanza cha Mombasa Diaries.
Kwa pamoja, wawili hao wamekuja na project ya kusaidia watu
kuweza ku,stay fit.. ‘Tukifanya work out
yetu ya kwanza Jumamosi iliyopita, ilikua ni kwa ajili ya wake wa watu maarufu
tu, ilikua tumepanga tuwe tunaifanya kila jumamosi kuanzia saa tisa jioni hadi
saa kumi na mbili jioni. Lakini tangu tulipoanza kupost picha za work out ya
kwanza, watu wengi wametaka kujiunga na programme hio hivyo basi si ya watu
maarufu tu bali kila mtu ambaye atakua anataka kufanya mazoezi’ Archy amenieleza.
‘Kila mtu ambaye ana interest ya kuwa fit #TukutaneNyaliBeach kila siku ya
Jumamosi kuanzia saa tisa. Sisi sote ni vijana, si vizuri watu wawe na miili
ambaye hawawezi kujivunia pale wajiangaliapo kwenye kio wakiwa peke yao.’ Kaa La Moto ambaye ndiye anayeendesha
mazoezi hayo amemalizia na kusema ya kwamba watakao kua wanataka kujiunga
wawasiliane na Archy Kawera kwa
kubonyeza [[ HAPA ]]
NB;
VibeCity Awards Mombasa zitafanyika hivi karibuni, na washabiki
wanaoshiriki kupiga kura wanapata fursa ya kushinda airtime kati ya
kshs.100 na kshs.1000. Washindi 10 kila siku kwa kupiga kura [HAPA]
Good job Kaa la moto and the blogger as well .thumbs up
ReplyDelete