Kijana Anayetatiza Mabinti Mombasa

Kama kawaida ya wanamitindo wengi duniani, mwanamitindo huyu ambaye nyota yake inazidi kung'aa kila uchao amekua akiwakosesha usingizi mabinti, si Mombasa tu bali kutoka sehemu tofauti humu nchini kwani katika katika account zake za mitandao ya kijamii kumejaa jumbe kutoka kwa mabiniti wakiomba mda nayeye.
Mwanzo mwa mwezi huu, Abdultwalib Swaggaf aliweza kushinda tuzo ya Mwanamitindo Bora Wa Kiume Wa Mwaka katika tuzo za Mombasa Awards 2016. Mbali na kua mwanamitindo, Saggaf anaendelea na masomo ya shahada ya International Business Studies katika chuo kikuu cha U.S.I.U. Ni mwandishi hodari kwani anamiliki blog ambayo hua anaangazia maswala mbalimbali kama vile mapenzi, mitindo, dini, maisha ya kawaida na kuchambua sinema. Kando na uanamitindo, uandishi na masomo, vilevile Abdultwalib anajihusisha sana na mchezo wa soka na anachezea klabu ya Bodo Glimt Mombasa.
Katika mtandao wa Instagram(saggaf93) mwanamitindo huyu ana zaidi ya followers 15,000.... jambo ambalo anajivunia kwani mwenyewe anasema si rahisi kufikisha followers wengi kiasi hicho ndio maana hua anathamini kila anayemfollow na ni haohao mashabiki ndio walioweza kumfanya ashinde tuzo ya Mombasa Awards2016 na anaamini ya kwamba bado ni mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii kama vile facebook ndio watakaomsaidia kuweza kushinda tuzo ya Face Of Mombasa katika tuzo za VibeCity Awards Mombasa ambazo kura zinaendelea na watu wanapiga kura [[ HAPA ]]

 NB; VibeCity Awards Mombasa zitafanyika hivi karibuni, na washabiki wanaoshiriki kupiga kura wanapata fursa ya kushinda airtime kati ya kshs.100 na kshs.1000. Washindi 10 kila siku kwa kupiga kura [HAPA]

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele