Mbona Wasanii Wa Nyumbani Hulipwa Pesa Finyu? Amz, Totti Na Dazlah Wafunguka

Awamu iliyopita kulikua na malalamishi kutoka kwa wasanii flani kutoka mombasa kwamba kulikua na upendeleo katika mfumo wa kuwachagua wasanii watakao tumbuiza. Mwaka huu lawama ambazo zimesambaa baadi ya tamasha hilo kukamilika ni kwamba wasanii wageni walilipwa hela ndefu zaidi kuliko wasanii wa nyumbani ambao kulingana na walalamishi ni kwamba ndio walifaa kupata mgao mkubwa katika tamasha hilo.
Ni swala ambalo limezua mjadala mtandaoni na  Kelvin Jilani/Mtu Bei alionelea awatafute baadhi ya washikadau wakuu wa sanaa ya Mombasa kupata maoni yao kuhusu issue hii na akafanikiwa kuongea na Producer Totti, Dazlah pamoja na Amz Tempoz. 
Totti akiongea amesema 'sisi wenyewe tuna promote mziki wao kila mahali hivyo basi mwishowe wanajizolea umaarufu na ndio maana wanaitwa kwenye hizi shows.....mimi naweza sema sisi wenyewe hatusapoti mziki wetu, wale jamaa wanachezwa saana kule kwao wanapata shows za hela nyingi ndio maana wana invest kwenye mziki wao, huwezi mlipa msanii 30k alafu utarajie afanye video ya milioni moja'' 
Amz naye akasema, '..kitu kinachoangusha mziki wa pwani ni kwamba wasanii wa mziki pwani hawajathaminiwa. Wanafaa kuthaminiwa kwanza kuanzia ngazi za serikali hadi kwa mashabiki.' Amz amesema kuwa mziki unafaa upewe heshima kama mojawapo ya kazi kubwa saana nchini....''Wale watu wanakuja kupiga show huku ni kwa sababu kule kwao wamethaminiwa ndio maana sisi nasi tunawathamini''
Msanii Dazlah naye kasema kuwa malipo ya shows yanategemea na maelewano ya mtu binafsi...''kitambo msanii wa nje ametoka huko aje kupiga show anataka pesa nyingi ni kwa sababu ya maelewano,ukiambiwa utalipwa 20k ukubali upige show alafu baadae ulalamike ni makosa saana''  Skiliza mahojiano yote kamili [[ HAPA ]]
 NB; VibeCity Awards Mombasa zitafanyika hivi karibuni, na washabiki wanaoshiriki kupiga kura wanapata fursa ya kushinda airtime kati ya kshs.100 na kshs.1000. Washindi 10 kila siku kwa kupiga kura [HAPA]


Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele