WCB Wasafi Kufanya Kazi Na Msanii Huyu Wa Mombasa
Ndio label inayohit sana Afrika Mashariki kwa sana. Wasanii walioko katika label hii ni moja
kati ya wasanii ghali kuwapata. Mwishoni
mwa wiki jana, muanzilishi wa WCB,
Diamond Platinumz alikua nchini Kenya kwani alikua na show mjini Meru.
Msanii kutoka Mombasa ambaye anatamba na wimbo wake wa NYOTA YANGU, Jay Madini ni mmoja kati ya watu waliochukua fursa hio ya safari ya Diamond nchini Kenya kufikia management
hio na kupanga makubwa. Akiwa na promoter wake, Morris Mbetsa, walikua na
mkutano wa zaidi ya masaa mawili na manager wa WCB, Sallam TK na kupanga mambo makubwa.
‘Nashkuru tuliweza
kukubaliana na Wasafi kitu ambacho tulikua tunataka. Ni project inayonihusu
mimi na WCB. Sitazungumza kwa kina kwa
sasa kwa sababu kuna mengi zaidi tunafaa tuyapange na WCB ndio kuwe na mwelekeo mwafaka. Baada ya hapo ndio tutapeana details vizuri’ Jay alieleza meza yetu ya habari.
Msanii huyo ambaye tayari amerudi mjini Mombasa anajiandaa kutayarisha video yake mwishoni mwa wiki hii na
pia management yake ikishirikiana na Mzazi
Willy M Tuva wa Mseto EA ambayo
watakua wanazindua surprise project hivi karibuni.
Comments
Post a Comment