Bawazir Awaponda Wasanii Wa HipHop Kutoka Pwani
Msanii ambaye anatamba na track yake mpya ya OBI MAMA, iko [[ HAPA ]]amesema ya kwamba bado
hajaona msanii mkali wa hiphop kutoka pwani.
Msanii huyu ambaye amekua akigonga vichwa vya habari haswaa kila
anapotumbuiza jukwaani kwani hua anashabikiwa si mchezo amesema hayo baada ya
kuskiza wimbo uliofanywa na magwiji 9 wa hiphop kutoka pwani (Someone Somewhere Remix), iko [[HAPA]]
‘Kusema ukweli hawa
wasanii wa hiphop wanaibisha Sanaa hapa pwani. Hebu skiliza ule wimbo abayo
wameufanya, yani ni kutapatapa tu ndio wamefanya. Hakuna mistari mizito, hakuna
hata mmoja aliyeonyesha uwezo wa kuteka track, wamemuaibisha tu producer.’ Bawazir amesema.
Akisistiza kauli yake Bawazir
amesema ya kwamba ukiskiza track nyingi za hiphop hapa pwani utaskia jinsi
ma,producer wanavyojikakamua kuandaa mziki wenye ubora lakini wasanii wanatetereke
tu kwenye nyimbo zao.
‘Hata heri hao wa Nairobi wanaowadharau wakisema ya
kwamba hawajui mziki lakini mwisho wa
siku wanaonyesha ukomavu katika track zao. Coast hiphop artiste should pull up their socks au sivyo watabaki
tu kuskiza wabana pua wanachojua Zaidi ni kuwekeana beef tu.’ Bawazir amemalizia.
Comments
Post a Comment