Kibibi Salim Ampeleka Susumila Kortini Baada Ya Kutalakiana

Kibibi Salim ambaye ni mke wa msanii Susumila amempeleka kortini msanii huyo baada ya kutalakiana na msanii huyo.
Kibibi ambaye aliandikiwa talaka Septemba 4 amemfikisha msanii huyo kortini ili ahakikishe ya kwamba msanii huyo anawajibika kwa malezi ya mtoto wao Halima aka Susumilaress.
 'Nilipewa talaka tatu na Susumila na nimeenda kortini ili kuhakikisha ya kwamba anashuhulikia malezi ya mwanangu. Na kingine kilichonifanya niende kortini ni kutaka eda. Katika sheria za kiislamu wanandoa wanapotalakiana, mume anafaa aendelee kuwajiba kama bwana kwa mda wa miezi mitatu kwa kua huenda watu wakaskizana na kurudiana tena.' Kibibi ameeleza.

Wanandoa hao ambao tangu waingie katika ndoa wamekua wakigonga vichwa vya habari kwa sababu mbalimbali kama vile Kibibi kushtumiwa ya kwamba alimnyakua Susumila kutoka kwa mwanamke mwengine.
'Siongelei hio issue kwa sasa' ndio jibu la Susumila alilonipa nilipojaribu kumhoji kuhusu kutalakiana kwake na Kibibi ambaye hawajafikisha hata mwaka tangu waoane. Wawili hao ambao walioana Oktoba 22, 2015 wamekataa kufunguka sababu iliyowafanya kutalakiana.

Comments

  1. Ndio dunia hii tuliambiwa tukue watu wazima tuyaone tulidhani ni maembe.Pole kakangu Susumila yusuf mitihani tu!

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele