Mrundiko Wa Vitambulisho Wazidi Kua Kero
Mrundiko wa
vitambulisho umeendelea kuongezeka katika ofisi mbalimbali za usajili wa kitaifa kote nchini. Mrundiko huo
umekua ukiongezeka kila uchao baada ya shirika hilo kuboresha huduma za kutoa
stakabadhi hizo.
Mfano ni Jane Kimenju, serial number- 243395256, ambaye alikua katika ofisi
ya Huduma Centre hii leo kuchukua
kitambulisho chake, alituma maombi ya kitambulisho 22 Agosti 2016, kitambulisho chake kiliweza kutolewa Septemba 1 na ameweza kukipata
alipofika ofisini hapo.
Katika ofisi
ya Mombasa ya Huduma Centre, kuna mrundiko wa vitambulisho Zaidi ya 4,000 ambavyo vinasubiri wenyewe
kuvichukua. Vilevile katika ofisi ya Bima
Towers, kuna Zaidi ya vitambulisho 5,300
ambavyo pia havijachukuliwa na wenyewe.
Katika ofisi
hizo ambazo hushuhudia vitambulisho Zaidi ya 300 kuchukuliwa kila siku, wanaowasilisha maombi ya vitambolisho
huvipata wiki 3 tu baada ya kuwasilisha maombi.
Shirika hilo
linazidi kupeana vitambulisho 30,000
kila siku nchini ila cha kusikitisha ni kwamba wengi wanaotuma maombi ya
vitambulisho hivyo hawajishuhulishi tena kufuatilia vitambulisho hivyo.
Mrundiko huo
wa vitambulisha unaonyesha jinsi watu walivyowepesi wa kulalamikia serikali
wakisema ya kwamba serikali haiwajibiki ilhali ni hao wenyewe ndio
hawashuhuliki kufuatilia mambo wanayolalamikia. Swala hili
la vitambulisho limekua swala nyeti kwa mda kwani kumekua na mamalimishi ya
kwamba kuna sehemu zengine za nchi zimezuiliwa kupeana vitambulisho kwa
maksudi, madai ambayo ukiangalia kwa kina hayanai ukweli kwani hata wanaofanya
kazi za usajili wa vitambulisho katika ofisi hizo ni wa kutoka sehemu mbali mbali humu nchini.
Shirika la
kitaifa la usajili linaomba kila aliyetuma ombi la kitambulisho afike ofisini
ili kuchukua stakabadhi hizo muhimu hususan eneo la Pwani ambalo linaongoza katika mrudiko huo wa vitambulisho katika
ofisi mbalimbali.
Comments
Post a Comment