Nyota Ndogo Akataa Zawadi Ya Milioni 16

 
Msanii Nyota Ndogo alimshangaza mumewe baada ya kukata bonge zawadi siku ya Jumamosi. Msanii huyo alikua amepangiwa bonge la surprise na mumewe huyo ambaye walifunga pingu za maisha miezi minne iliyopita lakini akaipiga na chini offer hio.
Nyota Ndogo alikua ameambiwa ya kwamba wanaenda matembezi mafupi siku ya jumamosi, kumbe alikua anapelekwa showroom kununuliwa gari mpya. Nielsen ambaye ndio mume wa Nyota Ndogo alimchagulia Nyota gari ya shilingi milioni 16 lakini Nyota Ndogo akakataa!
"Mume wangu alikua amenipeleka kuninunulia gari ya milioni 16 lakini nikakataa. Gari hio ilikua ni yangu ya kutumia nikiwa Denmark lakini nikakataa. Sioni kama nahitaji kua na gari Denmark kwa sababu tayari niko na gari Kenya." Nyota Ndogo ameeleza.
"Nilionelea ni heri hizo pesa tujenge nyumba Mombasa tuwe na nyumba mbili, Voi na Mombasa na tujenge nyumba kadhaa za kupanga ambazo zitatupa mapato kuliko gari ambayo haileti mapato. Sitaki mwanangu awe Kenya Kimbo, nimyonye pesa alafu afilisike, nilimpenda yeye wala si pesa ndio maana nataka tujenge maisha yetu ya mbeleni sitaki tutumie pesa alafu tuje tuteseke." Nyota Ndogo amemalizia huku akisema ya kwamba mumewake anapanga kuja kuishi Kenya pindi tu atakapo staafu

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele