Kaa La Moto Amjia Juu Gates Mgenge Hadharani

 Msanii mkali wa hiphop, jamaa ambaye vilevile yuko kwenye team ya Karate ya Kenya na ana bleckbelt amemjia Juu presenter wa Pilipili FM wa kipindi cha MwakeMwakeLive, Gates Mgenge.

Kaa La Moto ambaye ame,upload picha ya Gates akiwa jukwaani ameshikilia kipaza sauti huku ametinga tshirt nyeusi iliyoandikwa ALLAH AKBAR, ameandika na kumwambia mtangazaji huyo ya kwamba hio ndio tshirt kali ambayo ashawahi kuivaa, imebeba ujumbe mzuri, ALLAH AKBAR ambayo inamaanisha ya kwamba Mungu ni mkubwa ila akamkanya asithubutu kuingia nayo club au eneo lolote la anasa labda iwapo tu atakua ameziba maandishi hayo.


Nikauliambayo Gates ame,comment akijaribu kupingana na Kaa lakini mashabiki hawakumpa nafasi kwani wengi walionyesha kumuunga mkono Kaa La Moto. Wengi waliomuunga mkono msanii huyo wamedai ya kwamba sisawa kuingia na nguo hio katika eneo lolote la anasa au hata msalani kwasababu kulingana na dini yakiislamu sisahihi kuingia na kitu chochote cha kumtukuza Mungu katika sehemu hizo wakati wale waliokua wanamuunga mkono Gates wamedai ya kwamba ni nguo tu ya kawaida na haina makosa kumsifu Mungu mahali popote pale.
-Kupigia kura blog hii katika tuzo za Pwani Celebrity Awards2016, tuma ujumbe 24C kuenda kwa 21195 ..shukran!

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele