'KARIBU MOMBASANI' Yapokelewa Kwa Kishindo

 
Hatimaye msanii Benso ameachia ile track ambayo ameitengeneza kwa ajili ya kusifu mji wa Mombasa. Track hio ambayo amewashirikisha Kigoto na GeeGee na imetayarishwa na Producer BeatsBoy pamoja na Producer Shirko. Ni track kali sana ambayo amesifia uzuri wa mandhari ya Mombasa na raha zilizopo Mombasa.
Baada ya kuiachia rasmi tu track hio, ndani ya masaa mawili downloads za wimbo huozilikua zimefika zaidi ya elfu moja. Ishara nzuri sana yakufanya vizuri kwa wimbo huo kwani  hua ni nadra sana video/wimbo kutoka pwani ya Kenya kupata download/views zaidi ya 2000 katika siku ya kwanza.
Kufanya vizuri kwa track hio bado kumepatwa na pigo kwani kuna 'wajanja' wa mitandaoni ambao wameamua hawatakaa wakitazama mafanikio ya wimbo huo na wakafanya 'ujanja' wao na kuingia katika website ya msanii ( www.ngomakenya.co.ke ) huyo na kuufuta wimbo huo.
 
Tukienda hewani, mafundi walikua wanashuhulikia kudhibiti website hio kwa kuongeza security ya website hio kabla kuurudisha tena mtandaoni wimbo huo ambao kwa sasa unaweza kuuskiliza na kutazama video ya mashairi ya wimbo huo hapa chini..



Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele