Hizi Ni Ishara Ya Kwamba MC Tucker Ni 'iLLuminati' Au?
Kumewahi kua na uvumi kwa mda sasa ya kwamba MC Tucker aka Tucker The Entertainer ni mwanachama na mshiriki wa nguvu za giza. Ni uvumi ambao uliniacha na maswali sana, mbona watu wanasema ya kwamba Tucker ni illuminati? Au jamaa amenunua gari niniii? au ghafla bin vuu Tucker amenunua mjengo wa kufa mtu? Ikanibidi angalau nipitie katika kurasa zake za mitandao ya kujamii nipate fununu kabla kumhoji kuhusu madai haya....
Nilichokiona pia kiliacha na maswali zaidi, kwani nilipata ya kwamba katika picha kadhaa ambazo Mc Tucker amewahi kuzipost akiwa ameonyesha ishara kadhaa ambazo zinakisiwa kutumika na wafuasi wa 'illuminati'. Ilibidi nimtafute Tucker mwenyewe atueleze kulikoni na ishara hizi anazozitumia.
'Watu wanasema tu lakini kitu ambacho hawajui ni kwamba naamini Mungu sana na siwezi jihusisha na nguvu za giza. Ishara ambazo nafanya nikipiga picha ni mapozi tu ila hazina maana yoyote. Mimi si illuminati na siwezi kuwa illuminati.' Tucker amefunguka akisistiza ya kwamba yeye haamini nguvu za giza hata kidogo.

Izaaaa Mungu Pekeee
ReplyDeleteilluminut direct to
ReplyDelete