Je Kaunti Ya Mombasa Inastahili Kiwango Hiki Cha Mgao Wa Taifa Au Inanyanyaswa?
Serikali kuu imetangaza kiwango cha pesa iliyopangia kila kauntikwamwakawa2017/18. kati ya kaunti zilizopangiwa kupewa kiwango kikubwa cha pesa ni kaunti ya Nairobi-billioni 17.9, Meru-bilioni 12, Nakuru-bilioni10.4, Machakos-bilioni 8.6, Kisumu bilioni 7.3 na Mombasa bilioni 6.9.
Mombasa ndio mji mkuu wa pilikatika nchi hii ya Kenya lakini katika mgao huo imetengewa kiasi kidogo zaidi kuliko kaunti ya Meru, Nakuru na hata Machakos. Nairobi ambayo ndio mji mkuu waimepangiwa takriban bilioni 18 ilhali Mombasa ni takriban bilioni 7, ambayo imegawiwa pesa takriban mara tatu zaidi ya Mombasa.
Bandari ya Mombasa inaingizia nchi takriban bilioni 36 kwa mwaka, pesa ambazo huenda moja kwa moja katika serikali kuu na kiwango kilichotengewa kaunti ya Mombasa hakifiki hata asilimia 20 ya kipato cha bandari ya Mombasa, mbona kaunti ya Mombasa isitengewe japo asilimia 30?
Je itakuaje wakati reli ya kisasa inayoendelea kujengwa SGR itakapokamilika na containers kuanza kufanyiwa clearing Naivasha? Je ni kwamba Mombasa inastahili kupewa kiwango kidogocha pesa kuliko kaunti ya Meru na Nakuru au ni hujma ya kichinichini kutaka kufanya kaunti ya Mombasa isiwe na maendeleo kwa kua asilimia kubwa ya wapiga kura wamekua wakiunga mkono chama cha upinzani cha ODM na uongozi wa kaunti ya Mombasa, Gavana Ali Hassan Joho amekua mstari wa mbele kupinga uongozi wa Jubilee ?

Comments
Post a Comment