Wasojali Band Kutuzwa Zaidi Baada Ya Kushinda Tuzo Tatu Kwa Mpigo
Katika tuzo za Pwani Celebrity Awards2016 ambazo zilifanyika katika hoteli ya English Point, Wasojali Band walionyesha ubabe baada ya kunyakua tuzo zote ambazo walikua wameteuliwa kushindania.
Wasojali Band ambao wako katika management ya Kubwa Entertainment waliweza kujizolea tuzo tatu usiku huo, yote hayo yakiwezeshwa na wimbo wao NITALIA NAWE ambao walioshirikisha Kelechi Africana ambaye pia naye yupo katika Kubwa Entertainment. Wimbo huo uliweza kushinda katika kitengo cha Collaboration Of The Year na Video Of The Year na baadae wakafunga kazi katika category ya Group Of The Year.
Akiongea baada ya tuzo hizo, Athman Baba ambaye ni mmiliki wa Kubwa Entertainment amesema ya kwamba vijana wake wamekua wakifanya kazi kwa sana na wameonyesha ya kwamba wanaweza na kwa kua waliweza kushinda tuzo hizo tatu, yeye mwenyewe pia anawapa bonge la 'treat'.
'Kwanza nashukuru sana kwa kila mtu kwa sababu wamewapokea Wasojali na Kelechi vizuri sana na support yao ndio imetufikisha hapa. Kuna vitu vingi vizuri vinakuja mwanzoni mwa mwaka ujao ila kabla tuviachie naona niwape zawadi hawa vijana kwa kushinda tuzo hizi.' Athman amesema
'Nitawapeleka katika kisiwa flani hivi wakapumzike angalau kwa wiki mbili hivi. Sitataja ni kisiwa gani kwa sasa kwa sababu nataka iwe surprise kwao lakini ni Kenya au Tanzania.' Athman amemalizia na kuahidi ya kwamba atahakikisha ya kwamba mwaka ujao Wasojali Band watafanya kazi kubwa zaidi ya mwaka huu na ana imani ya kwamba mambo yakienda kama yalivyopangwa kwa sasa basi 2017 utakua mwaka mwengine mkubwa kwao.

Comments
Post a Comment