Dazlah Aongelea Kuhusu Tuhuma Za Ku,copy Wimbo Wa Chege Na CDiamond Platnumz
Msanii Dazlah amefunguka na kuwahakikishia mashabiki wake kuwa bado yuko imara na wanafaa kutarajia mengi kutoka kwake. Hii ni baada ya mmoja ya mashabiki wake kumuuliza kwa nini hatoi hits mfano wa Kidekide iliyofanya vizuri sana. Kulingana na Dazlah ni kwamba tangu atoe Kidekide ametoa hits nyingi sana lakini kwa vile Kidekide bado haijaisha mtaani, imekua vigumu sana kwa mashabiki kuzikubali track hizo. Vilevile, Dazlah amedai ya kwamba yeye hurekodi kila siku na kapuni ana nyimbo zaidi ya mia mbili ambazo hajaziachia bado.
"Tangu nitoe Kidekide sijakaa serious nikasema eti nafanya ngoma kwa maana nilikua nashughulikia mambo flani kuweka ma,dancers wangu sawa, kutengeneza ofisi yangu na Chilemonde, kwa hivyo sikutaka kukaa kimya ndio maana nikatoa ngoma kadhaa hapa katikati kama vile Nitalia na Ringa". Je anazizungumziaje tuhuma za kukopi wimbo wa Diamond Platinumz na Chege-Waache Waoane kwenye ngoma yake ya Waache Waongee? Msikilize Dazlah akifunguka katika mahojiano yake na Kelvin Jilani / Mtu Bei >>HAPA
Comments
Post a Comment