DJ Lenium Afunga Harusi Tena (Photos)

Amekua katika sanaa ya mziki kwa takriban miaka kumi na tatu sasa na anajivunia kuwa na tuzo kumi kutoka kwa kazi zake tofauti anazofanya katika tasnia ya burudani ikiwa uigizaji, ku,mc, utangazaji, na u,DJ.
Ikiwa leo ni siku ya 9, Disemba, mkongwe huyu katika sanaa ya burudani katika eneo la pwani amefanya sherehe ya kuadhimisha miaka mitano tangu afunge pingu za maisha na mkewe, Maureen Angira ambaye wamejaaliwa watoto wawili pamoja.
 
Sherehe hio ambayo imefanyika katika kanisa ya St Stephens ACK Bamburi, ilihudhuriwa na marafiki kidogo sana na familia. 'Si rahisi kuona mtu ambaye yuko katika sanaa, haswa dj kudumu sana katika ndoa. Nashkuru sana kufikisha miaka mitano katika ndoa na ndio maana nikachukua ya ku,renew vows tena kanisani kwa kua nachukulia serious ndoa yangu na familia yangu.' Dj huyo ameeleza huku akionyesha wingi wa furaha.
 
Kutoka Machampali Media, tunamtakia DJ Lenium na Maureen amani katika ndoa yao na iendelee kudumu. Hizi hapa ni baadhi ya picha kutoka kwa sherehe hio...
 

Comments

  1. Hongera....Mola azidi idumisha ndoa yenu

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele