Kurushiana Makonde Kati Ya Susumila Na Wazo Baba Kwasitisha Shoot Ya Video Yao
Siku ya Jumatatu, msanii Wazo Baba ndio alikua ameachia wimbo wake wa LINDA aliomshirikisha Susumila, pia ndio siku ambayo walikua wana,shoot video ya wimbo huo.
Wakiendelea ku,shoot video hio, ilifika katika scene moja ambayo wasanii hao wawili walikua waingize ni kama wanapigania mwanamke. Katika ku,shoot scene hio, Wazo Baba kwa bahati mbaya alim,wahi Susumila ngumi ya ukweli, kwa uchungu aliouskia naye Susumila akalipiza kimaksudi ngumi ya ukweli kwa Wazo Baba. Stori ikabadilika sasa, scene ya kuigiza kwa video ikawa ndio uwanja wa ndondi.
Ilibidi waliokuwepo waingilie kati kuwatenganisha lakini tayari wawili hao walikua wametoana damu. Walipotenganishwa tu, Susumila alifululiza hadi alipokua ameegesha dereva wake na kumwambia waondoke. Juhudi za watu kujaribu kumtuliza Susumila na kumuomba asiondoke katika shoot hio ziliambulia patupu na kupelekea kukatishwa kwa utayarishaji wa video.
'Ilikua bahati mbaya tu. Katika ile hali ya kuigiza, kuvutana nkajisahau na kwa bahati mbaya ngumi moja nikaiskuma kwa nguvu kwa mwenzangu Susumila. Nafkiri ilimuumiza kwa sababu alinilipiza kwa hasira na ndio tukaanza kupigana. Ni kitu ambacho najutia kwa kweli kwa sababu haikua maksudi na ni kitu ambacho kimenitia hasara kwa sababu nilishalipia video na hata nilikua nimegharamia director Ricky Bekko na crew yake kuja kuandaa video hio na ilibidi warudi Nairobi bila kufanya kitu. Nimejaribu kumfikia Susumila lakini ameni,block kila mahali. ' Wazo Baba ameeleza.
Wimbo ambao ulikua unatayarishiwa video uko >>HAPA
Wajinga wote wawili
ReplyDelete