Matonya Ataja Wasanii Watatu Kutoka Mombasa Ambao Anawakubali Sana

Matonya ni mkongwe  wa bongofleva  ambaye alianza  kushika  anga za mziki  katika miaka ya 2005  na wimbo wake wa Vaileti. Ni zaidi ya miaka kumi sasa tangu aanze kupenya anga za juu za mziki na, style zinaenda zikibadilika na  jinsi ya kufanya mziki kubadilika lakini ameweza ku,maintain na kurudi tena katika chati za mziki na kuweza kushindana tena na wanamziki ambao wameibuka  na ari na mbinu mpya.
Matonya ambaye yupo mjini Mombasa alifunguka katika mahojiano yake na blog hii kuhusu siri iliyomuwezesha kuduma  katika game   na  kuweza kurudi  tena baada ya  kukaa kimya kwa mda. Vile vile Matonya amewataja wasanii watatu ambao anawakubali kutoka eneo la pwani.
'Kusema ukweli wasanii ni wengi sana lakini kuna huyu msanii anaitwa Susumila namkubali sana. Pia Chikuzee nampenda sana. Paneli pia ni msanii ambaye namkubali na tayari niko na collabo naye na ntakua nashoot video naye wikendi hii. Ila Susumila na Chikuzee ni wasanii ambao wanajituma sana na napenda sana juhudi zao. Hawa  ni  wasanii  ambao wakinitafuta katika  mda huu ambao niko  Mombasa tunaweza kufanya kazi nao.'  Matonya  ambaye    atakua  na  show mjini Watamu sku ya  Jumamosi ameeleza  ya kwamba mbali na mashabiki wa pwani ya Kenya kupenda sana mziki  wa bongo, nchini   Tanzania   pia mzikiwa Mombasa hua  unachezwa  sana. Je  ni kiu gani  ambacho  kinawasaidi wasanii   wa bongo  kuweza kupendwa sana  nchini  mwaonahata   nje?   Msikilize   hitmaker huyowa  SUGUA BENCHI  akifunguka zaidi  >>HAPA

Comments

  1. thats true... also Dazlah na Kaa La Moto wako juu...

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele