Mmoja Wa Wasanii Wenye Bidii Zaidi Kutoka Pwani


Ukiweka kando kidogo wasanii ambao tayari wamejipa majina, kuna wasanii ambao ndio wanakua. Hilo ndio kundi ambalo la wasanii ambao wanahitaji nguvu sana ilikupenya kwa sababu waliotangulia tayari washajitengenezea soko na haiwachukui nguvu nyingi kuskuma kazi zao tofauti na hawa ambao ndio bado wanajaribu kutengeneza connections mbili tatu na kujifunza vitu kadhaa katika sanaa na biashara ya mziki.
 
Kati ya fungu hilo la wasanii, Mombasa kuna msanii Romromy ambaye anaonyesha kukua kwa kasi kwani ana bidii ya mchwa. Baada ya kutoa track yake ya kwanza ya 'Hapa Kenya' na baadae 'Ujaluo Utaniua', Romromy ameamua hatapumzika kwani tayari ameachia video yake mpya ya 'End Month'  ambayo audio yake imeatayarishwa na Naiboi/Pacho Entertainment. Kwa mwendo huu na kujitahidi kufanya kazi ni ishara tosha ya kwamba Romromy ni mmoja ya wasanii ambao ni wakuangalia na kutarajia vitu vikubwa sana mwaka wa 2017... Hii hapa ni video yake mpya..

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele