PDay Na Producer Khalid Wafunguka Kuhusu Khalid Kukataa Kutoa Video Ya PDay Kisa Madem Wabovu
‘…Wale mademu uliolea
walikua wabovu kwa hivyo tafta wengine na venue nyingine tu,shoot tena…’
ni kipande cha post ambayo Pday alipost
katika mtandao wa facebook akidai ya kwamba Producer Khalid wa A Miliion
Records/Vision amemdhulumu pesa zake baada ya ku,shoot video alafu baadae
akamgeuzia lugha na kudai ya kwamba vixen waaliotumiwa walikua wabomu kwa hivyo
video inafaa kurudiwa tena. PDay ambaye anaonekana mwingi wa hasira amefunguka
kwa kina kuhusu madai hayo ya kutapeliwa na Producer Khalid kwa kueleza
mpangilio wao wa kazi hio ulikuaje kuanzia mwanzo hadi sasa kufikia kudaiana
mitandaoni katika mahojiano yake na Kelvin Jilani/Mtu Bei >> HAPA
Khalid naye ambaye amedai ya kwamba Pday ni mtu asiyekua na
shukrani na anatafuta kiki na pengine ametamani kupata likes na comments za
facebook ndio maana anafanya anayofanya.
‘Ni kweli alileta mademu ambao wamechoka
lakini hio si sababu ya mimi kuzuia video yake, nilikua nampa ushauri tu…Video
yake ataipata baada ya 1 hour tu akimaliza balance . Pday anaongea kuhusu video
wakati haongei kuhusu deni’….
Producer Khalid pia ameeleza jinsi walivyoelewana na
walivyofanya kazi na yaliyojiri katika
utayarishaji wa video hio hadi kufikishana walipofikishana. Mskilize Producer
Khalid akifunguka kwa kina >> HAPA
Comments
Post a Comment