Susumila Ampoteza Babake

Hitmaker wa Tuliza Nyavu, msanii Susumila ambaye alimpoteza mamake mzazi mnamo 2014 amepata pigo tena kwa kumpoteza babake mzazi. Mzee Kombo Kinando Tangai ambaye ni mkaazi wa Chumani alikua na umri wa takriban miaka 70. Akinieleza habari hizo, Susumila ameeleza ya kwamba mzee Kombo aliugua kwa mda mrefu kabla ya kuaga dunia asubui ya leo.
'Mzee ametuacha asubui ya leo. Bado tunaendelea na mipango ya mazishi lakini kuna uwezekano mkubwa ya kwamba tutampumzisha Jumamosi hii ya tarehe 24 nyumbani Chumani. ' Susumila amesema.
Tunawapa pole familia ya marehemu Mzee Kombo, Mungu awajaalie wepesi katika wakati huu mgumu na ampumzishe mwenda zake kwa amani.

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele