Fat S Aacha Kuuza CD Na Kuanza Kuuza Mayai Ferry

Msanii Fat S amekua gumzo kwa mda mrefu kwa biashara yake ya kujiuzia CD katika kivukio cha Likoni. Wengi wamekua wakisema ya kwamba shida nyingi na kukosa hela ndiko kunakomsukuma msanii huyo kujiuzia CD zake ferry jambo ambalo amelikana akidai ya kwamba kuuza CD ferry kunampa kipato kikubwa zaidi ya biashara yeyote anayoweza kufikiria kufanya kwa sababu kwa siku hawezi kukosa kuingizi takriban Kshs. 20,000 mfukoni.
Ila katika siku za hivi karibuni Fat S amezua kizungumkuti. Hio ni baada ya kuonekana akiuza mayai badala ya cd katika kivukio hicho. Kwa mda wa takriban wiki mbili sasa, msanii huyo ameonekana kutupilia mbali kuuza CD na kukita kuuza mayai yakuchemshwa.
Baada ya kupata picha kadhaa za msanii huyo akiendelea na biashara hio,meza yetu ya habari imejaribu kumfikia msanii huyo ila amekua hapokei simu zetu wala kujibu hata ujumbe mmoja kati ya nyingi alizotumiwa.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele