Otile Brown Apigwa Marufuku Kutumia Nyimbo Zake
Siku moja tu baada ya kutangaza kujitoa katika management ya
DreamLand Music, management hio
imetoa maamuzi yao ambayo yanaonekana kuwa pigo kubwa sana kwa msanii huyo.
Kupitia mtandao wa kijamii,aliyekua manager wa Otile Brown, Dr Eddie ametangaza ya kwamba nyimbo 10 aliokua amefanya Otile Brown ni mali ya Dreamland Music na ni marufuku kwa
msanii huyo kuzitumia mahali popote kibiashara kwa sababu msanii huyo hahusiani
tena na management hio.
Kauli na maamuzi hayo ni pigo kwa msanii huyo
kwani hio inamaanisha ya kwamba kufikia sasa msanii huyo hana wimbo au video
aambayo anaweza kufanya kazi nayo hivyo basi kumaanisha ya kwamba msaanii huyo
atakua anaaanza upya kabisa.
Comments
Post a Comment