Otile Brown Atengana Na Dr Eddie (DreamLand Music)
Wiki moja tu baada ya manager wake kufuta video zake katika
mtandao wa Youtube, hitmaker wa Dejavu, Otile
Brown ametangaza kuachana na management ya Dreamland Music inayomilikiwa na Dr Eddie.
Wakati video zake ilipoondolewa katika mtandao wa
Youtube, akiongea na mtandao mmoja
maarufu Afrima Mashariki, Otile Brown
alikiri na kusema ya kwamba kuna tofauti imeibuka baina yake na manager wake ila
anatarajia ya kwamba watasuluhisha katika siku za hivi karibuni. Ila inaonekana
tofauti zao zimeshindwa kusuluhishwa kwani mapema hii leo kupitia mitandao ya
kijamii, Otile Brown ametangaza ya
kwamba hayupo tnea chini ya uangalizi wa DreamLand
Music.
Japo hakueleza
kilichopelekea wawili hao kutengana, bali ameandika na kusema ya kwamba
hayupo tena Dreamland Music na
akahakikishia mashabiki wake ya kwamba hatowaangusha. Itakumbukwa ya kwamba, kabla video zaek kufutwa katika mtandao wa Youtube, Otile Brown ndiye msanii kutoka Pwani ambaye alikua na views nyingi katika video zake kwani hakuna video yake hata moja ambayo ilikua na views zilizopungua 300,000.
Comments
Post a Comment