Katika siku za hivi karibuni, katika hatua ya kujiongezea mashabiki haswaa katika jiji la Nairobi na Kenya nzima kwa ujumla, msanii Susumila amekua akifanya collabo na wasanii tajika kutoka jiji la Nairobi. Alianza na MAPEPE ambayo kulingana na yeye, hio ndio ilikua track yake iliyofanya vizuri zaidi mwaka wa 2016 alafu baadae akafanya WEWE aliomshirikisha Avril, wimbo ambao video yake ndio video ya Susumila ambayo imefanya vizuri zaidi katika mtandao wa Youtube. Ukiwa ni mwaka mpya sasa, msanii huyu ambaye anatarajiwa kufunga pingu za maisha mwezi wa Aprili, amemshiriikisha Timmy T Dat ambaye kwa sasa ndiye msanii anayepeta zaidi nchini Kenya. Ni wimbo ambao ulitayarishwa na Producer Totti. Kupata kuskiziliza na kupakua hit hio, bonyez>> HAPA