Mwanamitindo Kutoka Mombasa Avamiwa Na Kuuawa


Ni mwanamitindo kutoka Mombasa ambaye alikua anachipuka kwa kasi chini ya mwamvuli wa Shadow Models. Hapo jana mchana alikumbana na mauti akiwa nyumbani kwao maeneo ya Kizingo. Janet Asunah ambaye alipatikana akiwa tayari ameshaaga dunia nyumbani kwao alikua na jeraha la kichwa na kulingana na walioona eneo la tmukio inakisiwa ya kwamba huenda aligongwa kichwani na kuburutwa hadi chumba chake cha kulala.

''haijulikani kama kitendo hicho kilifanywa na mtu mmoja au zaidi kwa sababu alikua peke yake nyumbani lakini kuna vitu kadhaa vimepatkana vimeibiwa kutoka kwake. Simu yake, decorder na viatu vipya pair mbili ambavyo alivinunua tu last week ndio vilikua vimeibiwa" Maria Jamal (Pwani Fashion Awards, Model Of The Year), ambaye ni rafiki yake wa karibu sana ameeleza.

Mipangi ya mazishi ya Janet ambaye ameacha mtoto wa miaka mitano inaendelea. Mungu amrehemu na Pole kwa familia, ndugu na marafiki, tunawaombea Mungu awape nguvu na wepesi katika wakati huu mgumu.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele