Kundi Alilounda Chikuzee Laingia Katika Mvutano Ambao Huenda Ukavunja Kundi Hilo



Chikuzee, C New na Producer B.I walikuja pamoja na kuunda kundi la Dossari International na kauchia video yao ya DUNIA NZIMA mwanzoni mwa mwezi wa Februari.
Baada ya kutangaza kuunda kwa kundi hilo, mashabiki walionyesha kua na imani sana na kundi hilo kwani wasanii wote watatu wameonyesha kua na uwezo na style yao ya Tam Tam flavaz imeonekana kugusa nyoyo za wengi. Ila huenda kundi hilo likawa kundi la ‘one hit wonder’ kwani  huenda likavunjika wakati wowote iwapo mvutano uliopo utakosa kutatuliwa.
Mvutano katika kundi hilo umesababishwa na management flani  kutoka jinini Nairobi. Wakiwa katika media tour ili ku,promote video yao mpya, waliweza kufuatwa na management hio ili kundi hilo liwe likifanya kazi chini yake. Baada ya mazungumzo na management hio ambayo iliweza kueleza nia na mikakati yake ya kazi, wawili kati ya wasaniii hao watatu walikubali na mmoja akakataa  na kusababisha kutokuingia katika mkataba na management hio.
Msanii huyo aliyekataa kuingia kundi hilo kuingia katika makubaliano na management hio anadai ya kwamba management hio haina tofauti na zengine zilizotangulia kuchukua na kunyonya wasanii wa pwani na pia hao wenyewe tayari wana uwezo wa kujismamia huku wenzake wakisema ya kwamba mikakati ambayo management ilikua tayari kukubaliana nayo ilikua haitawakandamiza  na ingesaidia pakubwa kufikisha malengo ya kundi hilo.
Uwepo wa kundi hilo bado ni wa kubahatisha kwani wasanii hao wawili ambao wapo tayari kufanya kazi na management hio huenda wakamtimua mwenzao kutoka kundi hilo ili waingine katika makubaliano na management hio japo huenda ikawa vigumu kwani msanii huyo anayedinda amekua na mchango mkubwa sana katika kundi  hilo ambalo lilikua limepangiwa kufanya tour nchini Tanzania mwezi huu.

Comments

  1. Wasuluhishe jamani lisivunjike.

    ReplyDelete
  2. Msanii mkubwa kama Chikuzee bado hajui kwamba vikunde vina challenges mob????
    He could have just gone solo, that's my view though .

    ReplyDelete
  3. Kundi lisivunjwe tafadhali

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele