Kundi Alilounda Chikuzee Laingia Katika Mvutano Ambao Huenda Ukavunja Kundi Hilo
Chikuzee, C New na Producer B.I walikuja pamoja na kuunda
kundi la Dossari International na kauchia video yao ya DUNIA NZIMA mwanzoni mwa
mwezi wa Februari.
Baada ya kutangaza kuunda kwa kundi hilo, mashabiki
walionyesha kua na imani sana na kundi hilo kwani wasanii wote watatu
wameonyesha kua na uwezo na style yao ya Tam Tam flavaz imeonekana kugusa nyoyo
za wengi. Ila huenda kundi hilo likawa kundi la ‘one hit wonder’ kwani huenda likavunjika wakati wowote iwapo
mvutano uliopo utakosa kutatuliwa.
Mvutano katika kundi hilo umesababishwa na management
flani kutoka jinini Nairobi. Wakiwa
katika media tour ili ku,promote video yao mpya, waliweza kufuatwa na
management hio ili kundi hilo liwe likifanya kazi chini yake. Baada ya
mazungumzo na management hio ambayo iliweza kueleza nia na mikakati yake ya
kazi, wawili kati ya wasaniii hao watatu walikubali na mmoja akakataa na kusababisha kutokuingia katika mkataba na
management hio.
Msanii huyo aliyekataa kuingia kundi hilo kuingia katika
makubaliano na management hio anadai ya kwamba management hio haina tofauti na
zengine zilizotangulia kuchukua na kunyonya wasanii wa pwani na pia hao wenyewe
tayari wana uwezo wa kujismamia huku wenzake wakisema ya kwamba mikakati ambayo
management ilikua tayari kukubaliana nayo ilikua haitawakandamiza na ingesaidia pakubwa kufikisha malengo ya
kundi hilo.
Uwepo wa kundi hilo bado ni wa kubahatisha kwani wasanii hao
wawili ambao wapo tayari kufanya kazi na management hio huenda wakamtimua
mwenzao kutoka kundi hilo ili waingine katika makubaliano na management hio
japo huenda ikawa vigumu kwani msanii huyo anayedinda amekua na mchango mkubwa
sana katika kundi hilo ambalo lilikua limepangiwa kufanya tour nchini Tanzania mwezi huu.
Wasuluhishe jamani lisivunjike.
ReplyDeleteMsanii mkubwa kama Chikuzee bado hajui kwamba vikunde vina challenges mob????
ReplyDeleteHe could have just gone solo, that's my view though .
Kundi lisivunjwe tafadhali
ReplyDeleteKizaazaa hicho
ReplyDelete