Msanii HustlaJay Atishia Kumlima Makonde Mtangazaji Billy Miya Kisa 'Socialite'



Msanii na mwanaharakati wa hiphop kutoka pwani ya Kenya, HustlaJay Maumau amemuonya mtangazaji Billy Miya wa Baraka FM ya kwamba atamlima makonde pindi tu watakapokutana . HustlaJay ametishia kumpa adabu mtangazaji huyo kwa kumcharaza makonde pindi watakapokutana sababu ikiwa ni socialite.
HustaJay amesema ya kwamba Billy Miya anafaa makonde ili apate nidhamu kwa sababu amekua akipotosha jamii. Kulingana na HustlaJay ni kwamba Billy Miya anapotosha jamii kwa kua manager wa Socialite ambaye ni LIZZ KHANYANJE. ‘Mbona asiwe manager wa mtu ambaye ni kioo na kielelezo kizuri kwa jamii? Mbona asiwe manager wa msanii au muigizaji? Mbona socialite? Hizi kazi za socialites tunazijua bwana kwa hivyo hizo biashara hatuzitaki sisi. Either aache ku,manage socialite na aombe msamaha kwa jamii la sivyo ile siku tutakapokutana basi nitamfunza adabu.’ HustlaJay amefoka kupitia mtandao wa Whatsapp katika kikundi cha ‘CoastShowbizz’.
Billy naye hakua na mengi ya kusema bali amemjibu na kumwambia HustlaJay ajaribu kile anaweza kadri ya uwezo wake na ndipo atakapojua ya kwamba kimya kina mshindo na utakua mwisho wake wa kuingiza pua yake katika biashara za watu.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele