Msanii HustlaJay Atishia Kumlima Makonde Mtangazaji Billy Miya Kisa 'Socialite'
Msanii na mwanaharakati wa hiphop kutoka pwani ya Kenya, HustlaJay Maumau amemuonya
mtangazaji Billy Miya wa Baraka FM ya kwamba atamlima makonde
pindi tu watakapokutana . HustlaJay ametishia kumpa adabu
mtangazaji huyo kwa kumcharaza makonde pindi watakapokutana sababu ikiwa ni
socialite.
HustaJay amesema
ya kwamba Billy Miya anafaa makonde
ili apate nidhamu kwa sababu amekua akipotosha jamii. Kulingana na HustlaJay ni kwamba Billy Miya anapotosha jamii kwa kua
manager wa Socialite ambaye ni LIZZ KHANYANJE. ‘Mbona asiwe manager wa mtu ambaye ni kioo
na kielelezo kizuri kwa jamii? Mbona asiwe manager wa msanii au muigizaji?
Mbona socialite? Hizi kazi za socialites tunazijua bwana kwa hivyo hizo
biashara hatuzitaki sisi. Either aache ku,manage socialite na aombe msamaha
kwa jamii la sivyo ile siku tutakapokutana basi nitamfunza adabu.’ HustlaJay amefoka kupitia mtandao wa
Whatsapp katika kikundi cha ‘CoastShowbizz’.
Billy naye hakua na mengi ya kusema bali amemjibu na
kumwambia HustlaJay ajaribu kile anaweza kadri ya uwezo wake na ndipo
atakapojua ya kwamba kimya kina mshindo na utakua mwisho wake wa kuingiza pua
yake katika biashara za watu.
Kumeharibika sio?
ReplyDeleteHahaha...makonde hatari.
ReplyDelete