Rapper mkali kutoka mtaa wa ilala Dar rees salam Chid Benz aepushwa kifungo cha miaka miwili gerezani na mama yake.Rapper huyo siku ya alhamisi alikua amehukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani au alipe f aini ya shillingi laki saba za tanzania ambapo mamake alimlipia faini hiyo iliyomuweka chidi huru uraiani tena. Hukumu hiyo ilitolewa baada ya chidi kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya sh. 38, 638, bangi yenye thamani ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo.Mnamo Februari 18 Chidi Benz aliwahi kukiri makosa yote matatu mbele ya Hakimu.