Mashabiki Wawaweka Roho Juu Dizzle Na Dogo Richie
Baada ya kufanya vizuri kwa wimbo KIFAA, ambao Dizzle alimshirikisha hitmaker wa Mziki Majanga , hatimaye wawili hao wameachia video hio ambayo ilikua imesubiriwa kwa hamu na gamu. Kulingana na wawili hao ni kwamba hawakua na nia ya kufanyia video wimbo huo lakini mashabiki ndio waliowaskuma kufanya hivyo. 'Baada ya kuachia KIFAA tu, nilikua nikiulizwa kila siku kama nitaachia lini video yake. Nikapuuza mwanzoni lakini mskumo kutoka kwa mashabiki ulizidi kwani idai ya wanaouliza swali hilo ikawa inaongezeka nikaona sina budi ila kuwapa wanachotaka kwa sababu mwisho wa siku huu mziki nafanyia mashabiki, na nafaa kuwapatia wanachohitaji .' Alielezea Dizzle wakati akitambulisha rasmi video hio iliyoongozwa na Ricky Bekko wa BigDreams . Itazame hapa...