Mwanamziki Wa Injili Kutoka Mombasa Anusurika Kifo
Mwanamziki wa kike wa Injili kutoka Pwani ambaye kwa sasa anawania tuzo mbili, ikiwemo Teenz Female Artiste Of The Year katika tuzo za Xtreem Awards na Female Gospel Artiste, Pwani Celebrity Awards2016, Sharon Shally nusura auwawe siku ya Jumamosi. Sharon ambaye alikua ametoka kazini maeneo ya Nyali alipatwa na mkasa huo katika eneo la Kengeleni/Lights takriban saa moja unusu usiku. Akingojea usafiri, Sharon alishtuka amebwagwa chini na amezungukwa na wanaume wanne ambao walikua wameshikilia mapanga na kumwambia akijaribu kusumbu tu huo ndio utakua mwisho wake. Uoga uliokua umemuingia ulimfanya asijue chakufanya ila tu kubaki akimuomba Mungu amuepushe kutoka mikononi mwa majambazi hao. 'Wangeweza kunifanya chochote kwa kua sikua na usaidizi wowote, ila nashkuru Mungu ni mkubwa. Walinipora kibeti, simu, pesa na stakabadhi zangu zilizokuwa katika kibeti hicho.' Ameeleza mwimbajihuyoambaye anasema hajawahi kupitia tukio la kuogofya katika ma...