Posts

Huwezi Fanya HipHop Kama Wewe Si Genius, Asema MamaLao

Image
Mkali wa uzito wa mistari na kufoka, Mamalao ambaye kwa sasa anafanya vizuri na track yake ya SUMU KALI ameweka wazi kuwa kilichomfanya akakita mizizi kwenye Hip hop ni kwa sababu ya msukumo wa kipaji huku sababu nyingine ikiwa ni kwamba wasanii wengi wa kike wameogopa kufanya hip hop hivyo ameamua kufanya hip hop ili kuwa mfano kwa wasanii wa kike. ''kwanza mimi nasema mziki wa hiphop ni mziki unaofanywa na watu wenye akili nyingi za ziada kwa sababu ukikaa chini ukiskiza hiphop utaskia maneno ambayo yanamgusa mtu kwa hivyo mtu anayefanya hiphop ni genius kwa kua anahitaji akili nyingi sana kuandika' '... amesema MamaLao Mamalao amewapa changamoto wasanii wa kike ya kujitokeza kwa wingi kufanya hip hop ili asiwe peke yake kwenye industry ya mziki wa huo. "yaani mimi nawambia wajitokeze kwa wingi maana endapo watanifanya mimi sina competition ya kutosha hapa coast watanifanya mimi mzembe" MamaLao pia amefunguka na kusema kwamba yuko single...je,...

Producer Totti na Producer Tee Waongelea Kuhusu Awards Za Hapa Pwani.. Kunani?

Image
Kila mtu anapofanya kazi nzuri hua anahisi vizuri pale anapotuzwa. Katika tasnia ya burudani hapa Pwani, tuzo ambazo zimekua zikiandaliwa zimekua zikipondwa sana kuliko kusifiwa. Watu wengi wamekua wakisema ya kwamba tuzo hizo hazina uwazi na zina mapendelea. Washika dau wengi wameshawahi kujiondoa katika tuzo kwa madai kua hawana imani nazo. Je ni kipi ambacho waandaaji wa tuzo hizi hua wanakosea na ni kipi wanaweza kufanya ili kurudisha imani katika tuzo za hapa Pwani ili watu waweze kuzithamini na kua na imani nazo. Hawa hapa ni Producer Totti na Producer Tee wakifunguka kwa kina kuhusu mtazamo wao kwa tuzo za hapa Pwani. Wasikilize HAPA

NEW MUSIC; Mr Blue Feat AliKiba - MBOGA SABA

Image
Vichwa viwili komavu vya bongofleva, Hitmaker wa Baki Na Mimi akiwa amemshirikisha star wa Aje wamekuja na hii mpya iliyotayarishwa na Producer Walter . Hawa wawili siku zote hua hawa,disapoint kna kwa hili jiwe jipwa pia wametisha ile mbaiya.. Ebu iskilize  HAPA

Mwanamitindo Kutoka Mombasa Avamiwa Na Kuuawa

Image
Ni mwanamitindo kutoka Mombasa ambaye alikua anachipuka kwa kasi chini ya mwamvuli wa Shadow Models. Hapo jana mchana alikumbana na mauti akiwa nyumbani kwao maeneo ya Kizingo. Janet Asunah ambaye alipatikana akiwa tayari ameshaaga dunia nyumbani kwao alikua na jeraha la kichwa na kulingana na walioona eneo la tmukio inakisiwa ya kwamba huenda aligongwa kichwani na kuburutwa hadi chumba chake cha kulala. ''haijulikani kama kitendo hicho kilifanywa na mtu mmoja au zaidi kwa sababu alikua peke yake nyumbani lakini kuna vitu kadhaa vimepatkana vimeibiwa kutoka kwake. Simu yake, decorder na viatu vipya pair mbili ambavyo alivinunua tu last week ndio vilikua vimeibiwa" Maria Jamal (Pwani Fashion Awards, Model Of The Year), ambaye ni rafiki yake wa karibu sana ameeleza. Mipangi ya mazishi ya Janet ambaye ameacha mtoto wa miaka mitano inaendelea. Mungu amrehemu na Pole kwa familia, ndugu na marafiki, tunawaombea Mungu awape nguvu na wepesi katika wakati huu mgumu. ...

Nyota Ndogo Aajiri Mrembeshaji Binafsi Baada Ya Masaibu Ya Vipodosi Katika Harusi Yake

Image
Taarifa za harusi yake zilipogonga vichwa vya habari, kilichoongelewa sana ni jinsi hitmaker huyo wa Watu Na Viatu alivyokua amepodolewa visivyo. Wengi waliweza kukosoa jinsi alivyokua amepakwa make up siku ya harusi wakisema ya kwamba ilikua haiendani na rangi ya ngozi yake na alikua anatisha. Tukio kama hilo huenda lisiwahi tokea tena kwani kuanzia hivi sasa, Nyota Ndogo ameajiri mrembeshaji binafsi ambaye atakua anamshuhulikia kuhusu mavazi na vipodozi katika kila tamasha atalokua anahudhuria, si Kenya tu bali hadi nje ya nchi. Kupitia Beryl Kawere, ambaye ni brand ambassador wa LAVIES SPA & BARBERSHOP (0720 325 364/ 0735 010 780 ) Nyali,  ambaye alikua harusini kwa Nyota Ndogo , aliweza kumualika Nyota Ndogo Katika salon hio na akafanyiwa make up na kurembeshwa nywele wakati wa photoshoot ya project yake inayokuja hivi karibuni. Nyota Ndogo alifurahishwa na kazi ya stylist huyo, Braxton #Tha_SalonGuybrax na akaamua ya kwamba huo ndio mwanzo mpya wa h...

NEW MUSIC: Mamalao Feat Johhny Skani-SUMU KALI

Image
Ni msanii wa hiphop kutoka Pwani ambaye anatisha sana kwa uwezo wake wakufoka na mistari yenye vinaa. Akiwa amemshirikisha mkongwe katika mziki hapa pwani, hitmaker wa Bembea, Johnny Skani , hii ni SUMU KALI, bonge la track leneye uzito lilioandaliw na Producer AMZ, Tempoz.  Listen / Download HERE

''Rihaha The Boss'' Atangaza Kugombea Ubunge Kilifi North

Image
Hashim Aida Omar ni mwanabiashara maarufu sana katika Kaunti ya Kilifi na Mombasa vilevile ila wengi wanamjua kwa jina la Rihaha The Boss , manager wa Susumila na pia juzi juzi aliwa,sign G uf Lyder, Kabambe, Dhilly Dhilly na Crash V . Ni mmiliki wa Rihaha Investments, kampuni ambayo inamiliki viwanda na kampuni kadhaa. Mwishoni mwa wiki jana, Rihaha alimfanyia bonge la harusi mmoja wa mfanyikazi wake kwa jina Khamisi. Ni sherehe iliyofanyika Rihaha Farm , nyumbani kwa Rihaha, Mtondia, Kilifi . Ni sherehe ambayo ilihudhuriwa na watu mbali mbali wakiwemo wanasiasa, wanabiashara na wasanii wengi. Katika sherehe hio, Rihaha alichukua fursa hio kutangaza ya kwamba amejitosa rasmi katika kinyang'anyiro cha 2017 na atakua ulingoli kumenyania ubunge katika eneo bunge la Kilifi North . ''wana Kilifi wajiandae kw amabadiliko kwani mambo nitakayoenda kuyafanya yatashangaza wengi... ni wakati wa Kilifi kuamka na kubadilika na maendseleo yafanyike...nitawajibika na k...