Posts

Showing posts from August, 2016

Tuzo Za Kifahari Za VibeCity Awards Zaanza Kufanyika

Image
Tuzo za kifahari za VibeCity Awards zinazodhaminiwa na Candy n Candy TV/Empire tayari zimeanza kufanyika. Tuzo hizo ambazo zitakua katika miji 6 mbalimbali hapa nchini zinatarajiwa kuwa za kiana yake kwani millionare Joe Kariuki anayemilikia Candy n Candy amesema ya kwamba lazima talanta zituzwe kwa level za kimataifa si kimzahamzaha tu. Wikendi hii, tuzo hizo zitakua zinafanyika mjini Eldoret. Maandalizi ya tamasha hilo kubwa  tayari yashaanza na tuzo zitakazopewa washindi tayari zishakamilika kwani zilikua zinatengenezwa na mmoja wa sonara maarufu jijini Nairobi. 'VibeCity Awards is not a joke na watu wataona. Tunaanza na Eldoret wikendi hii alafu baada ya huko tutatangaza ni wapi tutakua tunaenda kati ya Meru, Kisumu, Nakuru au Mombasa. The winners will celebrate, watu waendelee ku vote na ku,campaign because it is worth it' Joe ambaye mwishoni mwa wiki jana alishiriki katika Nanyuki Rally na kuibuka nambari 6 ameeleza . Mombasa ni moja ya miji iliyohusi...

Kaa La Moto Na Archy Kawere Waanzisha TKP (Toa Kitambi Project)

Image
Ni mmoja kati ya wasanii wakali wa Swahili hiphop hapa nchini. Uwezo wake wa kuchana kwa lugha ya Kiswahili umeweza kumfanya kupeperusha bendera ya hiphop hapa pwani. Kando na mziki, Kaa La Moto anajivunia kuwa katika timu ya taifa ya mchezo wa Karate . Aliposhirikiana na Sis P katika video yao ya wimbo ITS OK, alimsaidia pakubwa msanii huyo wa kike kufanya mazoezi ili kuwa na mwili wenye muonekano mzuri katika video hio.  Vilevile amekua na ukaribu na Archy Kawere ambaye ni mke wa msanii mkongwe wa hiphop hapa pwani, Johnny Skani   ambaye ni mmoja wa wahusika wa kipindi ambacho kimezua gumzo hata kabla kuanza cha Mombasa Diaries. Kwa pamoja, wawili hao wamekuja na project ya kusaidia watu kuweza ku,stay fit .. ‘Tukifanya work out yetu ya kwanza Jumamosi iliyopita, ilikua ni kwa ajili ya wake wa watu maarufu tu, ilikua tumepanga tuwe tunaifanya kila jumamosi kuanzia saa tisa jioni hadi saa kumi na mbili jioni. Lakini tangu tulipoanza kupost picha za work o...

WCB Wasafi Kufanya Kazi Na Msanii Huyu Wa Mombasa

Image
Ndio label inayohit sana Afrika Mashariki kwa sana. Wasanii walioko katika label hii ni moja kati ya wasanii ghali   kuwapata. Mwishoni mwa wiki jana, muanzilishi wa WCB, Diamond Platinumz alikua nchini Kenya kwani alikua na show mjini Meru. Msanii kutoka Mombasa ambaye anatamba na wimbo wake wa NYOTA YANGU, Jay Madini ni mmoja kati ya watu waliochukua fursa hio ya safari ya Diamond nchini Kenya kufikia management hio na kupanga makubwa. Akiwa na promoter wake, Morris    Mbetsa, walikua na mkutano wa zaidi ya masaa mawili na manager wa WCB, Sallam TK na kupanga mambo makubwa. ‘ Nashkuru tuliweza kukubaliana na Wasafi kitu ambacho tulikua tunataka. Ni project inayonihusu mimi na WCB . Sitazungumza kwa kina kwa sasa kwa sababu kuna mengi zaidi tunafaa tuyapange na WCB ndio kuwe na mwelekeo mwafaka. Baada ya   hapo ndio tutapeana details vizuri’ Jay alieleza meza yetu ya habari. Msanii huyo ambaye tayari amerudi mjini Mombasa anajiandaa kut...

Kijana Anayetatiza Mabinti Mombasa

Image
Kama kawaida ya wanamitindo wengi duniani, mwanamitindo huyu ambaye nyota yake inazidi kung'aa kila uchao amekua akiwakosesha usingizi mabinti, si Mombasa tu bali kutoka sehemu tofauti humu nchini kwani katika katika account zake za mitandao ya kijamii kumejaa jumbe kutoka kwa mabiniti wakiomba mda nayeye. Mwanzo mwa mwezi huu, Abdultwalib Swaggaf aliweza kushinda tuzo ya Mwanamitindo Bora Wa Kiume Wa Mwaka katika tuzo za Mombasa Awards 2016 . Mbali na kua mwanamitindo, Saggaf anaendelea na masomo ya shahada ya International Business Studies katika chuo kikuu cha U.S.I.U . Ni mwandishi hodari kwani anamiliki blog ambayo hua anaangazia maswala mbalimbali kama vile mapenzi, mitindo, dini, maisha ya kawaida na kuchambua sinema. Kando na uanamitindo, uandishi na masomo, vilevile Abdultwalib anajihusisha sana na mchezo wa soka na anachezea klabu ya Bodo Glimt Mombasa. Katika mtandao wa Instagram( saggaf93 ) mwanamitindo huyu ana zaidi ya followers 15,000 .... jambo ambalo a...

Beef Za Wasanii Wa HipHop Zilivunja Collabo Yao, Nyota Ndogo Na Afande Selle

Image
Msanii Nyota Ndogo ambaye kwa sasa anatamba na kibao cha Subira Yangu amesisitiza matamanio yake ya hapo awali ya kutaka kuwaleta pamoja wasanii wote wa hip hop na kuwashirikisha katika track moja. Katika siku za nyuma, Nyota aliwahi kuandika orodha ya wasanii wa HipHop kutoka Mombasa ambao angependa kuwashirikisha na kufikia kiwango cha hadi kuahidi kumjumuisha Afande Selle kwenye ngoma hiyo. Hata hivyo wazo hilo lilionekana kufifia huku mashabiki wakiachwa kwenye giza kuhusu haswa kilichosababisha kufeli kwa mradi huo. Leo hii Nyota ameweka wazi kilichosababisha kutofanyika kwa mradi huo alioupendekeza huku akisema alijaribu kivyovyote kuwafuata wasanii hao kuwasihi ila ikashindikana... 'Wasanii wa hiphop wanapenda saana kurushiana maneno hadi unashindwa utawa approach vipi,wale watu niliokua nimewachagua ambao nawaaminia hadi kuna mmoja nilimtaja jina niligundua kuwa wana chuki,sijui kama ni ya kutengeneza au ni ya ukweli lakini imeshindikana maana nakumbuka kuna mmo...

Mbona Wasanii Wa Nyumbani Hulipwa Pesa Finyu? Amz, Totti Na Dazlah Wafunguka

Image
Awamu iliyopita kulikua na malalamishi kutoka kwa wasanii flani kutoka mombasa kwamba kulikua na upendeleo katika mfumo wa kuwachagua wasanii watakao tumbuiza. Mwaka huu lawama ambazo zimesambaa baadi ya tamasha hilo kukamilika ni kwamba wasanii wageni walilipwa hela ndefu zaidi kuliko wasanii wa nyumbani ambao kulingana na walalamishi ni kwamba ndio walifaa kupata mgao mkubwa katika tamasha hilo. Ni swala ambalo limezua mjadala mtandaoni na  Kelvin Jilani/Mtu Bei alionelea awatafute baadhi ya washikadau wakuu wa sanaa ya Mombasa kupata maoni yao kuhusu issue hii na akafanikiwa kuongea na Producer Totti, Dazlah pamoja na Amz Tempoz.   Totti akiongea amesema 'sisi wenyewe tuna promote mziki wao kila mahali hivyo basi mwishowe wanajizolea umaarufu na ndio maana wanaitwa kwenye hizi shows.....mimi naweza sema sisi wenyewe hatusapoti mziki wetu, wale jamaa wanachezwa saana kule kwao wanapata shows za hela nyingi ndio maana wana invest kwenye mziki wao, huwezi mlipa msani...

Aomba Msamaha Baada Ya Mpenzi Wake Kuona SexTape Yake

Image
Si stori ya kweli bali ni kitu anachosimulia Kitole Kenda katika wimbo wake mpya wa DISMAIL . Jamaa aliachwa na mpenzi wake baada ya mpenzi huyo kutumiwa video ya mshkaji huyo akiwa na mchepuko wakifanya yao ya ndani. Katika wimbo huu jamaa anajaribu kuomba msamaha ili uhusiano urudi kama zamani baada ya kujitambua ya kwamba alikosa kumthamini mpenzi wake na kuchepuka.  Akiachia wimbo huu Kitole ameeleza ya kwamba jinsi watoto wa shule za upili wanavyochoma shule kulimfanya kuandika wimbo huo kwani wanafunzi hao wanaweza kueleza malalamishi yako kupitia ‘suggestion boxes’ na mitandao ya kijamii na wakaskika na sio kwa kuchoma shule. Pata hit hio mpya [[ HAPA ]]    NB; VibeCity Awards Mombasa zitafanyika hivi karibuni, na washabiki wanaoshiriki kupiga kura wanapata fursa ya kushinda airtime kati ya kshs.100 na kshs.1000. Washindi 10 kila siku kwa kupiga kura [ HAPA ]

Nyota Ndogo Aeleza Kwanini Aliolewa Na Mzungu

Image
Si wengi waliokuaa wanajua siku atakayofunga ndoa Mwanaisha Abdallah au ukipenda Nyota Ndogo ,  isipokua watu wachache tu ambao ni familia, ndugu na marafiki walioalikwa. Mbali na make up ya mwimbaji huyo wa Watu na viatu kua gumzo mitandaoni na katika vyombo vya habari baada ya picha za harusi kuachiwa, wengi pia walisemasema kuhusu mumewe Nyota Ndogo, Henning Nielsen kwa kua ni mzungu. Wengi walisema ya kwamba amemzidi umri, wengine wakasema ya kwamba ameolewa na mzungu kisa pesa.... Hapo jana Kelvin Jilani/MTU BEI akijitayarisha kufanya mahojiano na Nyota Ndogo aliwapa fursa mashabiki wamtupie maswali star huyo na shabiki mmoja, Erico Mbiko Allardyc   alitupia swali akiuliza "mbona aliamua kuoa ngozi nyeupe?". . 'Nilikua single kwa mda na wakati huo wote haun aliyeomba kunivisha pete. Ku,date nilidate na hata kuzalishwa lakini hata mmoja hakuna aliyesema will you marry me. Huyu baada ya kujuana naye kwa mda wa miaka miwili akaomba kunivisha pete, mbon...