Baada Ya Kukaa Korokoroni Kwa Wiki Mbili, Ability Wa Wasojali Band Aeleza Yaliyojiri
Ability ambaye ni mmoja wa kundi ya Wasojali Band ameeleza yaliyotokea hadi yeye kutupwa korokoroni kwa mda wa wiki mbili. Ability alitiwa mbaroni siku Februari 10 katika eneo la Mingira, Garsen wakati walipokua wanaelekea kupiga show Hola . ‘Ilikua siku ya Ijumaa na tulikua tunaelekea Hola kwa show yetu. Tulipofika katika roadblock ya Mingira, Garsen tukafanyiwa search na tukaambiwa tutoe vibali vyetu. Nilipotoa yangu wakaniambia ya kwamba ID yangu ni fake na wakaniweka katika ulinzi .’ Ability ameeleza. ‘Nilipokuja Kenya kutoka Tanzania nilikua hat sijafikisha miaka 18. Katika kupigapiga kazi nikaambiwa ya kwamba huenda nikatiwa mbaroni kwa kua sina kitambulisho. Aliyenieleza hayo akaniambia nikimpa hela flani ataniletea kitambulisho. Kwa kua mimi ni mgeni na skua najua kwamba kuna njia maalum ya kupata kitambulisho, nilipeana hela na baada ya siku mbili nikaletea kitambulisho nikajua hio issue nishamaliza. Ability amesimulia huku akiongeza na kusema ya kwamba ye...