Posts

NEW MUSIC: Wasojali Band-HAKUNA MATATA

Image
Ikiwa huu ni wakati ambao style ya band unashika na kuenea katika tasnia ya mziki wa Afrika Mashariki , Wasojali Band ni band ya hapa Mombasa inatesa anga za mziki si haba. Ni band ambayo ilituzwa tuzo ya band bora ya mwaka wa 2015 katika tuzo za Nzumari Classic Edition . Vijana ambao wako katika uangalizi wa Athman Babaz, hii hapa ni hit yao mpya iliyotayarishwa na Producer Noizer. DOWNLOAD/LISTEN HERE  

NEW VIDEO: Akothee Feat Diamond- MY SWEET LOVE

Image
Hii hapa ni collabo ya kwanza katika msanii kutoka eneo la pwani na jamaa ambaye ako juu sana Afrika Mashariki, Diamond aka Baba Tiffah . Akothee amemshirikisha Diamond katika Sweet Love, wimbo uliotayarishwa katika studio za Diamond-WCB Wasafi Records na Video imeongozwa na kuandaliwa na Godfather Production.

New Kid on the Block - Kelechi Africana

Image
Ni chipukizi ambaye anajipanga  kuja kutikisa anga za mziki. Anaenda kwa jina la Kelechi Africana. Chini ya uangalizi wa  Athman Babaz, anatarajiwa kuachia track yake ya kwanza kwa ijana Bomboribo. Ni track ambayo imetayarishwa na Producer Hammadoo wa Ghetto Records na Producer Noizer, GreenHouse Records

Jua watakao wakilisha Pwani katika tuzo za Bingwa Music Awards Mwaka Huu

Image
Tuzo za kila mwaka za ‪B ingwa Music Awards ‬ zinaingia msimu wake wa tatu tangu kuidhinishwa kwake. Tuzo hizo zinawaleta pamoja wasanii na wadau wa tasnia ya burudani kutoka ukanda wa Africa Mashariki ikiwemo Sudan Kusini na Rwanda . Wasanii wa hapa nyumbani hawakuachwa nyuma kwani nao wamo katika kinyang'anyiro hicho kwani wapo waliolteuliwa kwenye vitengo kuwania taji hizo wakipania kuongeza haiba zao kimziki. Nyota Ndogo, Mzee Ngala na SudiBoy na Dj Kaytrixx ni kati ya wale watakao peperusha bendera ya Pwa ni. Hii hapa list kamili ya walioteuliwa katika kila kitengo .     Bingwa Come Back Of The Year Nyota ndogo Wahu Wakimbizi DNA Abbass Octopizzo Bingwa Verse Of The Year Cannibal- welle welle rmx Sossun- Fimbo ya tatu Gabu- weka weka Dj Of The Year Kaytrixx Joe Mfalme Kriss Darlin Chokra(TZ) Shira(UG) Collabo Of The Year Sudiboy& Jaguar- barua kwa rais Welle welle rmx Avril & ommy dimpoz- hello Rabbit,Kristoff,frasha- ...

NEW MUSIC: Susumila Feat KingKaka-MAPEPE

Image
Toka 2007, amekua akiachia hit baada ya hit. Ni mmoja ya wasanii wakubwa na mkongwe hapa Pwani. Katika safari yake ya mziki hajawahi kupumzika au kukaa kimya. Nilimuuliza Susumila siri yake ya kuwa kwenye mziki kipindi kirefu bila kukimya wala kubuma ni nini na akasema ya kwamba  strategy na bidii ndio kila kitu. ''ukiwa na mikakati mizuri, ujue unachofanya na uwe focused, hakuna kitu kitakushinda. Mimi nimekua niki,change na trend na hio imenifanya ni,stay relevant katika mziki kwa kipindi hiki chote.'' Mwaka jana ulikua mzuri kwake na huu mwaka amesema hapunguzi mwendo, na kufungua mwaka hii hapa collabo yake na Rabbit aka King Kaka . Ni track iliyotayarishwa na Producer Totti aka La Internationale , Kay G Records. DOWNLOAD/LISTEN HERE

Susumila afunguka kuhusu uhusiano na Chikuzee, mipango yake ya 2016 na mengine zaidi

Image
Mwaka jana ulikua mwaka mzuri sana kwa Susumila. Ni mwaka ambao alitoa ngoma nyingi sana kwa mwaka mmoja zaidi ya mwanamziki mwengine hapa Pwani, si zake tu lakini kwa ujumla na zile alizoshirkishwa. Alikua na scandals kibao pia, kama vile mvutano na TK2, Kigoto na pia Chikuzee . Scandals zake hazikuishia katika kazi yake ya mziki tu bali pia maisha yake binafsi kwani kuachana na mama wa watoto wake na kufunga pingu za maisha na mwigizaji Kibibi Salim ilikua moja ya scandals ambazo zilitamba sana katika vyombo vya habari. Vipi uhusiano wake na Chikuzee ? Kuna uwezekano wa Collabo kati yao? Mwaka huu watu watarajie nini? mwendo ni ule ule kama wa mwaka jana au kuna mabadiliko gani atakua nayo katika kazi zake? Kwa maoni yake, ni wasanii gani wawili wakitoa wimbo utakua hit? MSIKILIZE SUSUMILA HAPA

Dogo Richie ana mipango gani mwaka huu?

Image
Dogo Richie aka Mr Yoyoba , hitmaker wa Sina Raha , jamaa asiyeishiwa na scandls, mwishoni mwa mwaka jana ali,sign,iwa na KingKong Entertainment alisema ya kwamba huu mwaka ni mwaka wake wakuuza sura? hivi alimaanisha nini? Mashabiki watarajie nini huu mwaka? Na swala la scandals analichukuliaje? Yeye kama msanii, ni msanii gani anamfagilia sana hapa Mkoani? Kwa maoni yake, ni wasanii gani anaamini wakifanya collabo hapa mkoani wata,hit balaaa? BONYEZA HAPA KUMSKILIZA DOGO RICHIE