Kutoka Tutu Band Ilikua Maamuzi Yangu Binafsi, Sikulazimishwa na Nyota Ndogo, Tatu Afunguka
Jina la msanii huyu mchanga lilijipata limezingirwa na utata wikendi iliyopita baada ya Juma Tutu ambaye ni kakake mkubwa kudai kuwa Tatu alikuwa amelazimishwa na dadake mkubwa ambaye ni Nyota Ndogo kutoka katika band ya Juma maarufu kama Tutu Band ambayo Tatu alikua akihudumu kama msanii pekee wa kike. Kulingana na Juma Tutu katika maandishi yake katika mtandao wa kijamii wikendi iliyopita ni kwamba nyota alimtoa Tatu katika bendi yake ili akamtaftie mume.Ilibidi tumtafute Tatu ili tupate kujua ukweli wa ndani kuhusu madai yote haya na kwa bahati nzuri binti tulimpata na akaweka kila kitu wazi.... "mimi sio mtoto mdogo mimi ni msichana mkubwa na nina maamuzi yangu binafsi" Huyu hapa Tatu katika mahojiano na Kelvin Jilani/ MTU BEI ...msikilize akifunguka mengi yanayohusu mipango yake ya kimuziki huku akikuonjesha wimbo wake mpya ushuhudie utam wa sauti yake. Bonyeza HAPA kusikiliza/Download