Hapo jana siku ya jumapili, 24-Julai Muwakilishi wa Wanawake wa kaunti ya Mombasa, Mishi Mboko aliweza kukabidhi wasanii kutoka Likoni, Talent House hundi ya Kshs. 500,000. Hundi hio ilitolewa wakati mheshimiwa Mishi Mboko alipokua akikabidhi mitaji/capital kwa makundi mbalimbali kutoka eneo la Likoni ili waanzishe mirandi itakayowapa uwezo wa kujitegemea na kujiendeleza kimaisha. Fisherman ambao ni mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo la wasanii, Talent House kutoka Likoni ameeleza ya kwamba hundi hio wameweza kukabidhiwa baada ya kuandika proposal takriban miezi mitano iliyopita na kuiwasilishwa katika ofisi za muwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Mombasa. ‘…Haikua mara yetu ya kwanza kuwasilisha proposal kwani tuliwahi kuwasilishwa proposal katika afisi ya mbunge wa Likoni, mheshimwa Mwahima na afisi mbalimbali lakini hazikuwahi kupitishwa. Ni vigumu kupata usaidi haswa kifedha kutoka kwa waheshimiwa unless uwe na proposal lakini bila hivyo hawaw...