Posts

Showing posts from November, 2016

Hii Ndio App Ya Kisasa Ambayo Hufai Kukosa Katika Simu Yako

Image
Simu za kisasa zimekua zikizidi kurahisisha kazi na maisha kila uchao. Moja ya vitu ambavyo vimekua vikiwezesha urahisi wa maisha kupitia simu za kisasa ni 'apps'. Kwa mfano, app ya uber ambayo imerahisisha katika usafiri. Na sasa kuna app mpya ambayo ilivumbuliwa na Michelle Kariuki , mwanadada ambaye ana miaka 18 tu. App hio ambayo inawekwa kama app nambari 4 duniani kwa sasa inarahisisha maisha kwa sana. Ni app ambayo inawezesha kupata kile utakacho kwa urahisi. Nikohub inaweza mtumiiazi kuletewa chakula, nguo, movie, vipodozi, vinywaji  mlangoni kwake. Ni app ambayo inajumuisha mauzaji wa bidhaa na huduma kadhaa kutoka maeneno mbalimbali hapa nchini. Watumiiaji wa Nikohub pia wanaweza ku,share picha kile walichoweza kukipata kupitia app hio kwa watumiaji wengine. Pengine ni huduma flani unatafuta na hujui utaipataje, Nikohub inakurahisishia kwani kulingana na mahala ulipo, utapewa options kadhaa wa jina na umbali wa kutoka ulipo hadi unapoweza kupata hudu...

Producer Totti Aeleza Wanachokifanya Ma,Producer 6 Walioungana

Image
Baadi ya ma,producer nguli Mombasa wakiwemo Teknixx, Amz, Tk2, Emmy Dee, Totti na Khalid hivi majuzi wameamua kuja na wazo la kuungana ili kuwa na maandamano ya kimawazo na kutayarisha kazi kadhaa pamoja. Kulingana na Totti ambaye ni mmoja kati ya maproducer hao ni kwamba, kila producer atachagua msanii kutoka kwa studio yake na kwa pamoja watakalia projects kadhaa za wasanii hao kwa lengo kubwa la kuleta mawazo pamoja na kutoa kazi nzuri. "Mashabiki kwa sasa wamegawanyika, kuna mashabiki wa studio flani na kuna mashabiki wa studio nyengine ndio tukaona tuje pamoja ili tuunganishe mashabiki wa studio mbalimbali... Tunachagua msanii flani kutoka studio flani alafu mwingine kwa studio nyingine alafu tunaona hawa wanaweza fanya hii style wanapiga." Totti ameeliza. Msikilize Producer Totti akiwataja baadhi ya wasanii ambao tayari wako kwenye mpango huo >> HAPA

Hizi Ni Ishara Ya Kwamba MC Tucker Ni 'iLLuminati' Au?

Image
  Kumewahi kua na uvumi kwa mda sasa ya kwamba MC Tucker aka Tucker The Entertainer ni mwanachama na mshiriki wa nguvu za giza. Ni uvumi ambao uliniacha na maswali sana, mbona watu wanasema ya kwamba Tucker ni illuminati? Au jamaa amenunua gari niniii? au ghafla bin vuu Tucker amenunua mjengo wa kufa mtu? Ikanibidi  angalau nipitie katika kurasa zake za mitandao ya kujamii nipate fununu kabla kumhoji kuhusu madai haya....   Nilichokiona pia kiliacha na maswali zaidi, kwani nilipata ya kwamba katika picha kadhaa ambazo Mc Tucker amewahi kuzipost akiwa ameonyesha ishara kadhaa ambazo zinakisiwa kutumika na wafuasi wa 'illuminati'. Ilibidi nimtafute Tucker mwenyewe atueleze kulikoni na ishara hizi anazozitumia.   'Watu wanasema tu lakini kitu ambacho hawajui ni kwamba naamini Mungu sana na siwezi jihusisha na nguvu za giza. Ishara ambazo nafanya nikipiga picha ni mapozi tu ila hazina maana yoyote. Mimi si illuminati na siwezi kuwa illuminati.' Tucker a...

Baada Ya Kupata Ufadhili Mpya, WAKASI wamerudi Tena Katika Sanaa Na Hii Mpya

Image
Wakasi ni mandugu walofatana, Abubakar Kitole(Safa) na Robert Mwadzidze(Roy) kutoka Kilifi. Walianza safari ya mziki mwaka wa 2010 mjini Malindi studio ya Terrbyte . Wameshawahi kufanya nyimbo kadha lakini hazikufanya vizuri kwa sababu ya kukosa ubora wa kiwango cha chini cha nyimbo hizo. Licha ya kutoka kwenye familia yenye hadhi ya chini lakini wamejaribu kueneza ujumbe wenye umuhimu katika jamii. Wamewahi kupewa ufadhili fulani ambao haukudumu kwa muda kwa sababu haukua unamuelekeo mzuri wa kuwanufaisha lakini baadae mwaka wa 2015 ndio walipata na Joseph Lewa mmoja wa shirika linalo toa ufadhili kwa mambo ya kimaisha ya kila siku kama elimu, talanta, magojwa ambaye aliamua kujitolea kuanza kuwapa support na kuendeleza safafri yao ya mziki na kuwapa uwezo wa kufanya track hii mpya katika studio za  Tee Hits . Kua wa kwanza kupata wimbo mpya wa MAPENZI MATAMU >>; HAPA

**Exclusive** Yaliyopangwa Kufanyika Stylus DJs Awards

Image
  Toleo la nne la tuzo za Stylus Djs Awards zimepangwa kufanyika siku ya 10 ya mwezi wa Disemba . Ni tuzo ku bwa nchini kwani ndio tuzo za kwanza Afrika nzima za Djs tu zikifuatwa na Ghana Djs Awards ambazo zilianza 2015 . Wakati mashabiki wakiendelea kupigia kura madj kupitia mtandao wa tuzo hizo HAPA waandalizi wa tuzo hizo wako mbioni kuhakikisha ya kwamba tamasha ya tuzo hizo litakua lakufana sanaaa. Kabla waandalizi wa tuzo hizo kupeana mipangilio halisi vya jinsi tamasha hilo litakavyokua, nimeweza kufanikiwa kupata habari za ndani ya kipi kilichopangwa kufanyika katika tuzo hizo... -Eneo la tukio litakua Mamba Village Centre, Nyali kuanzia saa kumi na mbili jioni (6pm) . -Setup za Djs haitakua moja wala mbili, lakini tatu....hio  ina maana ya kua mziki utakua uko  nyumbani,  ku,switch  kutoka dj mmoja hadi  mwingin...

Je Kaunti Ya Mombasa Inastahili Kiwango Hiki Cha Mgao Wa Taifa Au Inanyanyaswa?

Image
  Serikali kuu imetangaza kiwango cha pesa iliyopangia kila kauntikwamwakawa2017/18. kati ya kaunti zilizopangiwa kupewa kiwango kikubwa cha pesa ni kaunti ya Nairobi-billioni 17.9 , Meru-bilioni 12 , Nakuru-bilioni10.4 , Machakos-bilioni 8.6 , Kisumu bilioni 7.3 na Mombasa bilioni 6.9. Mombasa ndio mji mkuu wa pilikatika nchi hii ya Kenya lakini katika mgao huo imetengewa kiasi kidogo zaidi kuliko kaunti ya Meru, Nakuru na hata Machakos . Nairobi ambayo ndio mji mkuu waimepangiwa takriban bilioni 18 ilhali Mombasa ni takriban bilioni 7 , ambayo imegawiwa pesa takriban mara tatu zaidi ya Mombasa.  Bandari ya Mombasa inaingizia nchi takriban bilioni 36 kwa mwaka, pesa ambazo huenda moja kwa moja katika serikali kuu na kiwango kilichotengewa kaunti ya Mombasa hakifiki hata asilimia 20 ya kipato cha bandari ya Mombasa , mbona kaunti ya Mombasa isitengewe japo asilimia 30?   Je itakuaje wakati reli ya kisasa inayoendelea kujengwa SGR itakapokam...

Nomination List Ya Kenya Coast Music Awards2016

Image
Kwa mara nyengine tena, tuzo za kila mwaka za Kenya Coast Music Awards , zinazomilikiwa na Beyonce Promotions zimepangwa kufanyika tarehe 17 Disemba , Club Taurus . Ikiwa ni wiki moja tu baada ya washindi wa tuzo za Pwani Celebrity Awards2016 kutangazwa, hii hapa ni odhaya walioteuliwa kuwania tuzo hizo katika vitengo 27 tofauti 1. DANCE GROUP OF THE YEAR  a) JEKE JEKE  b) DABZ  c) B12  d) EXODUS  e) TSUNAMI  2. PROMISING ARTIST OF THE YEAR  a. Crazy K  b. CASH ERA  c. WYNAS  d. ZIKI  e. JAFARIZO  3. BLOGGER OF THE YEAR  a. MACHAMPALI  b. PWANI USANII  c. COAST NEWS  d. FRED MADEBE  4. GOSPEL SONG OF THE YEAR  a. FANYA – WILLY PAUL  b. MWEMA – MERCY MASIKA  c. UPENDO WAKO – BELLA  d. YAMENOGEA – RUTH MATETE  5. GOSPEL FEMALE ARTIST OF THE YEAR  a. MERCY MASIKA  b. MERCY D. LAI  c. C...

Baada Ya Willy Paul Na Size8 Kuja Na TW, Boss Kleva Naye Aja Na Yake

Image
Kwa siku tatu sasa, Willy Paul na Size8 wamekua gumzo sana baada ya kuachia video ya mpya ya TIGA WANA . Watu wamesifu sana ubora wa kazi hio ila pia kuiponda kwa kusema ya kwamba haikai ki,injili hata kidogo. Tukisalia katika sana ya mziki wa injili, hapa pwani kuna msanii Boss Kleva ambaye awali alikua akiijiita Bossyre lakini akabadilisha jina na kujiita Boss Kleva , ikiwa 'Boss' ni kutoka kwa jina lake ya Bosire na 'Kleva' kutoka jina lake pia la Clever. Ni msanii anayefanya mziki wa injili aina ya lingala na ameatuandalia video hii mpya ya Merci Nzambe (Asante Mungu) kwa ushirikiano wa producer tajika wa mziki wa injili, Dr. Eddie wa Dreamland Music Entertainment . Je ameweza kufikisha ujumbe wa injili au pia naye ameolea katika boti kama lile ya #TW .... hebu itazame hapa chini....

Orodha Kamili Ya Washindi Wa Tuzo Za Pwani Celebrity Awards2016

Image
Male Artist Of The Year         -Frankie Dee Female Artist of the Year   -Akothee New Artist of the Year       -Iddi singer Song of the Year      -Ting Go by Frankie Dee Video Of The Year       -Nitalia Nawe by Wasojali Band Feat Kelechi Africana Audio Producer of the Year        -Noizer        Video Director of the Year          -Bullet Stunnerz Collaboration of the Year        -Nitalia Nawe by Wasojali Band Feat Kelechi Africana Music Group / Band of the Year             -Wasojali Band          Male Gospel Artist Artist Of The Year              -Babje...

Hiki Ndicho Queen Renee Alichorudi Nacho Kutoka Tour Yake Nchini Ujerumani

Image
Mwaka ukianza, Queen Renee ali,launch album yake ya KAMATA CHAMPAGNE baada ya kumaliza tour yake ya miezi mitatu nchini Ujerumani na Switzerland. Amekua akiachia project kila mwezi tangu Februari , kama si video basi ni audio kutoka kwa album yake hio kabla kuenda kwa tour nyengine ya mwezi mmoja kuanzia mwezi wa October. Queen Renee ametua nyumbani na amekuja na project mpya ikiwa bado ni muendelezo wa album yake hio ya KAMATA CHAMPAGNE. Kabla hata kuchezwa katika kituo chochote  ha redio, umebahatika kuwa kati ya watu wa kwanza kupata wimbo huo uliotayarishwa na Producer Akeem .. Ipate>> HAPA

Amshirikisha Kidis Katika Hii Mpya Baada Ya Kimya Cha Mwaka Mmoja

Image
Aliachia wimbo wake wa mwisho 2015 na baadae kukaa kimya. Si kwamba mziki ulikua umemshinda ila alikua anajitafta na kupanga mbinu za kujiweka vizuri katika ramani ya mziki. Baada ya kimya hicho, Babza amevunja ukimya na TUWAPIGE BAO , track ambayo amemshirikisha Kidis The Jembe na ni mkono wa Producer TK2, Number 1 Records . Kua Wa kwanza kuskia wimbo huo >> HAPA

Wasojali Band Kutuzwa Zaidi Baada Ya Kushinda Tuzo Tatu Kwa Mpigo

Image
Katika tuzo za Pwani Celebrity Awards2016 ambazo zilifanyika katika hoteli ya English Point, Wasojali Band walionyesha ubabe baada ya kunyakua tuzo zote ambazo walikua wameteuliwa kushindania. Wasojali Band ambao wako katika management ya Kubwa Entertainment waliweza kujizolea tuzo tatu usiku huo, yote hayo yakiwezeshwa na wimbo wao NITALIA NAWE ambao walioshirikisha Kelechi Africana ambaye pia naye yupo katika Kubwa Entertainment . Wimbo huo uliweza kushinda katika kitengo cha Collaboration Of The Year na Video Of The Year na baadae wakafunga kazi katika category ya Group Of The Year . Akiongea baada ya tuzo hizo, Athman Baba ambaye ni mmiliki wa Kubwa Entertainment amesema ya kwamba vijana wake wamekua wakifanya kazi kwa sana na wameonyesha ya kwamba wanaweza na kwa kua waliweza kushinda tuzo hizo tatu, yeye mwenyewe pia anawapa bonge la 'treat'. 'Kwanza nashukuru sana kwa kila mtu kwa sababu wamewapokea Wasojali na Kelechi vizuri sana na support y...

Ratba Ya Ligi Kuu Ya Soka England Wikendi Hii

Image
Ni wiki ya kumi na mbili ya Ligi kuu ya soka nchini England . Kando na mechi inayosubiriwa kwa hamu na ghamu ambapo Manchester United watakua watakua wenyeji wa mahasimu wao wa mda mrefu na Arsenal , hii hapa ndio ratba kamili ya Ligi hio kwa saa za Afrika Mashariki .   Sat 19/11/16 Manchester United 3 : 30pm Arsenal Crystal Palace 6 : 00pm ...