Posts

Showing posts from September, 2016

Je Producer Amz Ana Beef Na Susumila Kwa Sababu Ya Wimbo 'Ngoma Imezima' ?

Image
Kama umechunguza kwa kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, Producer Amz amekua aki update list ya nyimbo ambazo alikua amepanga kuzitoa mwaka huu na moja wapo wa nyimbo hizi ilikuwepo "NGOMA IMEZIMA" ya Sususmila . Cha kushangaza ni kwamba wiki moja iliyopita Susumila ali,release Poster iliyoonyesha kuwa anaachilia t rack inayoitwa Ngoma Imezima ambayo kulingana na ujumbe wa poster ni kwamba imefanywa na Producer Totti, Kay G Records . Fununu zilitambaa kwamba hatua ya Susumila kutoa poster hiyo ilimkasirisha Amz kufikia hatua ya yeye kutoka kwa group ya whattsap ya 'Wachawi International.' Ili kutaka kujua ukweli, MTU BEI aliamua kumtafuta Producer Amz ambaye alifunguka kila kitu, Je ni kweli ya kwamba Amz yuko na beef na Susumila? Ebu sikiliza Amz akifunguka zaidi kuhusu issue hio katika link ifuatayo>> BONYEZA HAPA

Coast Most Expensive Model

Image
Ukihitajika utaje wanamitindo waliobobewa katika taaluma hio kutoka pwani listi yako haiwezi kuwa kamili iwapo itakosa mmiliki wa Fuschia Creativity. Ni mwanamitindo ambaye amekua katika industry kwa mda mrefu sana na kampuni yake ya Fuschia Creativity ndio iliyowafunza  uanamitindo watu maarufu kama vile Anita Nzaro, Ruthalia Michaels, Catherine Mage, Sandra Shantel na wengine wengi.   Dya Candy kama anavyojulikana ni mwanamitindo ghali zaidi katika eneo la pwani. Mwanamitindo huyu ambaye ili kuweza kumshirikisha katika kazi zako, lazima uwe una mkwanja mrefu na pia kazi zako ziwe na viwango vya kueleweka. Dya ambaye amebobea katika mambo ya vipodozi anamekua akipondoa washirikia katika vipindi mbali mbali kama vile NIRA, KELELE FM na kadhalika. Vilevile Dya ndiye mhusika mkuu katika mavazi ya co-host wa Mseto EA, Anita Nzaro. Benso, Daddy Owen na BigPin ni baadhi ya wasanii ambao amefanya kazi nao katika siku za hivi karibuni. 'Katika hii kazi lazimu ujue ku...

Escobar Ataja Wanaom'bania Asipate Shows

Image
Msanii ambaye alikua amepotea sana katika sanaa kwa mda mrefu na sasa amerudi akipambana arudi mahali alipokua amefunguka na kusema kinachomfanya yeye kukosekana katika tamasha kubwakubwa. 'Jiulize ni kwanini Chikuzee alikua akipiga show za kaunti alipokua na Susumila na walipokosana hapewi tena zile show... Vile vile Kigoto hapigi show, Kidis naye pia' Escobar amesema. Akiongea ndani ya kipindi cha chachawiza Bahari FM kwenye mahojiano na Pascal Shanga na Farida Ali , Escobar amesema kuwa kuna kundi la watu ambalo linadhibiti industry ya matamasha pwani.   Kulingana na Escobar ni kwamba ili kupata shows kubwa za makampuni ni lazima uhakikishe unajenga urafiki na kundi hilo la sivyo utaambulia patupu. Katika mchakato huu, Escobar ametoa mfano wa wasanii kama vile Kidis, Kigoto na Chikuzee kama baadhi ya wale walioathirika pakubwa na hali hii. Kuskiza jinsi Escobar alivyofunguka kwa kina katika mahojiano hayo [[ BONYEZA KATIKA MANENO HAYA ]]

Aah! Kumbe Hata Archy Kawere Aliimbiwa Wimbo Na Iddi Singer

Image
Zile fununu za Archy Kawere kutoka na msanii Iddi Singer zinadiki kupewa uhai kila kukuona. Baada ya ukaribu wao kua gumzo hadi watu kushuku ya kwamba wawili hao zile 'bae' na 'beib' zao si za mitandaoni tu kumefichuka ya kwamba wimbo mpya wa Iddi Singer ametungiwa mwanadada huyo.  Nimemtafta Iddi Singer kumuuliza kuhusu uvumi huu na ana haya ya kusema 'ukiskia huo wimbo waona Je....., yeye au waonaje?' ... Swali ambalo mimi binafsi nimeshindwa kulijibu labda nikutupie wewe msomaji unisaidie kupata jibu katika wimbo wenyewe ambao unaweza kuupatata katika mabano yafuatayo [[ WIMBO ANAUPATA UKIBONYEZA HAPA ]]

Aachia Video Iliyomgharimu Laki Tatu

Image
Baada ya kuachia wimbo mpya mpya wiki moja iliyopita, Dizzle sasa amekuja na video ya track yake hio ya pili baada ya kurudi katika mziki. Video hio ambayo iliandalaiwa na Director X Antonio ilimgharimu msanii huyu zaidi ya Kshs 300,000. 'Niliamua nigharamike kwa sababu nilikua nataka kitu cha uhahika, mziki umebadilika na lazima kama mtu anataka kutoboa basi hafai kufanya vitu kikawaida'  Dizzle ameeleza. Akifafanua zaidi kuhusu gharama hizo za video hio, Dizzle amesema ya kwamba aligharamia kila kitu katika video kuanzia location hadi mavazi ya walishirikishwa. Nguo ambazo zilivaliwa na kila mtu alizinunua yeye kwa kua alikua anataka muonekano mzuri katika video yake. Vixens waliotumika katika vdeo pia waligharamiwa usafiri wao kutoka maeneo mbalimbali wakiwa wametoka Malindi, Mombasa na Nairobi . Vilevile vixens hao hawakua wanauza sura tu katika video hio bali walikua kazi hivyo basi ilibidi walipwe vizuri iliwafanye kazi yao vizuri. Itazame video hio hapa chin...

Is Archy Kawere Cheating With An Upcoming Singer?

Image
Katikati siku za hivi karibu  kumekua na minong'ono ya kwamba huenda mke wa mwanamziki mkongwe hapa pwani Archy Kawere,   akiwa anacheza mechi za nje na msanii chipukizi anayekua kwa kasi,  hit maker wa NI WEWE,  Iddi Singer. Uvumi huo umeletwa na ukaribu ambao wawili hao wamekua nao katika siku za hivi karibuni kwani wamekua wakionekana katika mikahawa mbalimbali wakiwa pamoja. Isitoshe, wamewahi kufanya photoshoot pamoja mara kadhaa na hata mwishoni mwa wiki jana, siku ya Jumamosi, wawili hao waliandamana wakati msanii huyo alipokua anaenda katikati shooting ya kipindi cha Mseto EA ambako walionekana katika mapozi tatanishi   na pia kuitana majina ya mapenzi na kubembelezana kama vile Bae na beib mitandaoni. Nikimuuliza  Archy  kuhusu  uvumi huu amejibu  na kusema ya kwamba nimuulize swali hilo mwishoni mwa wiki.Naye Iddi nilipomuuliza kuhusu swala hilo alisema ya kwamba hajibu swali lolote isipokua maswali yanayohusu mzi...

NEW MUSIC: Wasojali Band - WACHA WASEME

Image
Video yao ya AUMBORA , iko [[ HAPA ]] bado inavurugavuruga anga za mziki na watu bado hawajapumua tayari vijana haw waliochini ya uangalizi wa Kubwa Entertainment wameangusha pini jipya. Wameonyesha uwezo mkubwa wa utunzi na sauti si haba, alafu producer Noizer wa GreenHouse RTecords ameitendea haki track hii ambayo unaweza kuipata [[ HAPA ]]

Nyota Ndogo Akataa Zawadi Ya Milioni 16

Image
  Msanii Nyota Ndogo alimshangaza mumewe baada ya kukata bonge zawadi siku ya Jumamosi. Msanii huyo alikua amepangiwa bonge la surprise na mumewe huyo ambaye walifunga pingu za maisha miezi minne iliyopita lakini akaipiga na chini offer hio. Nyota Ndogo alikua ameambiwa ya kwamba wanaenda matembezi mafupi siku ya jumamosi, kumbe alikua anapelekwa showroom kununuliwa gari mpya. Nielsen ambaye ndio mume wa Nyota Ndogo alimchagulia Nyota gari ya shilingi milioni 16 lakini  Nyota Ndogo akakataa! "Mume wangu alikua amenipeleka kuninunulia gari ya milioni 16 lakini nikakataa. Gari hio ilikua ni yangu ya kutumia nikiwa Denmark lakini nikakataa. Sioni kama nahitaji kua na gari Denmark kwa sababu tayari niko na gari Kenya." Nyota Ndogo ameeleza. "Nilionelea ni heri hizo pesa tujenge nyumba Mombasa tuwe na nyumba mbili, Voi na Mombasa na tujenge nyumba kadhaa za kupanga ambazo zitatupa mapato kuliko gari ambayo haileti mapato. Sitaki mwanangu awe Kenya Kimbo...

Aanza Tena Mziki Baada Ya Track Zake 6 Za Kwanza Kubuma

Image
Ni msanii ambaye anakuja vizuri na style ya hiphop. Ni mgeni katika sanaa ila si kwa sana kwani ashawahi fanya track sita ila zote amezitupia kapuni na kuanza upya. Hio ni baada ya kuona ya kwamba alikua anafanya mziki kikawaida sana na mda umebadilika. Akiachia track hii mpya aliyomshirikisha Producer wake Jimmy Ngalla, CHIBO D alisema ya kwamba anahesabu track hii kama ya kwanza kwani track alizofanya mbeleni alikua amezifanya kiholelaholela na asingefinga kokote ila kwa sasa safari yake ndio imeanza na wimbo huoa alioufanya katika studio za Frere Town Studio. upate [[ HAPA ]]

Bawazir Awaponda Wasanii Wa HipHop Kutoka Pwani

Image
Msanii ambaye anatamba na track yake mpya ya  OBI MAMA , iko [[  HAPA ]]amesema ya kwamba bado hajaona msanii mkali wa hiphop kutoka pwani.   Msanii huyu ambaye amekua akigonga vichwa vya habari haswaa kila anapotumbuiza jukwaani kwani hua anashabikiwa si mchezo amesema hayo baada ya kuskiza wimbo uliofanywa na magwiji 9 wa hiphop kutoka pwani ( Someone Somewhere Remix ), iko [[ HAPA ]]   ‘Kusema ukweli hawa wasanii wa hiphop wanaibisha Sanaa hapa pwani. Hebu skiliza ule wimbo abayo wameufanya, yani ni kutapatapa tu ndio wamefanya. Hakuna mistari mizito, hakuna hata mmoja aliyeonyesha uwezo wa kuteka track, wamemuaibisha tu producer.’ Bawazir amesema. Akisistiza kauli yake Bawazir amesema ya kwamba ukiskiza track nyingi za hiphop hapa pwani utaskia jinsi ma,producer wanavyojikakamua kuandaa mziki wenye ubora lakini wasanii wanatetereke tu kwenye nyimbo zao. ‘Hata heri hao wa Nairobi wanaowadharau wakisema ya kwamba hawajui mziki   lakini m...

The Mistery Of Uncollected ID Cards

Image
Identity cards continue piling up in registration offices in coast. I was surprised when officers working with registration bureau intimated me that they have 50,000 identity cards in the whole of coast. A spot check at Mombasa Huduma revealed that they have over 4000 identity cards. The regional office Bima has more than   5300. In these offices more than 300 cards are collected every day. Id cards are processed within the timelines. For instance I made a lady in Huduma Centre who had applied an id card 22 nd August 2016 by 1 st September 2016 the id had already come out. The registration office in Nairobi is processing 30,000 cards every day.   It is important that wananchi should collect identity cards after making applications. Sometimes I wonder when people claim that there is discrimination in id production and that the government is not fulfilling its mandate of issuing identification documents to the people yet the pile up of id cards is shockin...

Mrundiko Wa Vitambulisho Wazidi Kua Kero

Image
Mrundiko wa vitambulisho umeendelea kuongezeka katika ofisi mbalimbali   za usajili wa kitaifa kote nchini. Mrundiko huo umekua ukiongezeka kila uchao baada ya shirika hilo kuboresha huduma za kutoa stakabadhi hizo. Katika ofisi ya Mombasa ya Huduma Centre, kuna mrundiko wa vitambulisho Zaidi ya 4,000 ambavyo vinasubiri wenyewe kuvichukua. Vilevile katika ofisi ya Bima Towers, kuna Zaidi ya vitambulisho 5,300 ambavyo pia havijachukuliwa na wenyewe. Katika ofisi hizo ambazo hushuhudia vitambulisho Zaidi ya 300 kuchukuliwa kila siku, wanaowasilisha maombi ya vitambolisho huvipata wiki 3 tu baada ya kuwasilisha maombi. Mfano ni Jane Kimenju , serial number- 243395256 , ambaye alikua katika ofisi ya Huduma Centre hii leo kuchukua kitambulisho chake, alituma maombi ya kitambulisho 22 Agosti 2016, kitambulisho chake kiliweza kutolewa Septemba 1 na ameweza kukipata alipofika ofisini hapo. Shirika hilo linazidi kupeana vitambulisho 30,000 kila siku nchini il...

Wasanii 9 Wa HipHop Waweka Mbali Beef Zao Na Kuachia Collabo Hii

Image
Ni juzijuzi tu ndiuo Nyota Ndogo alisimulia jinsi beef za wasanii wa hiphop walivyotimua collabo ambaye alikua amepanga kati yake, wasaniii hao na msanii mkongwe wa bongo, Afande Selle [  ISOME HAPA ] kwani nusura wengine walimane makonde. Producer mkali, Amz ameweza kufanya jambo hilo gumu ambalo limekua likiwashinda wengi, kuwaweka wasanii wanaoshindana na wasioelewana katika track moja. Aliwezaje? Hadi ilipoachiwa, hakuna msanii hata mmoja ambaye alikua anajua ni msanii yupi mwengine atakua katika track hio. Yani ilikua ni siri ya Amz pekee ya kua ni nani na nani walikua watakua katika track hio kwani hakuna kati yao aliyeskia kilichorekodiwa hadi siku ya kuachia waimbo huu. Track hii ambayo imesheheni vichwa vikali vya hiphop toka pwani-  Kaa La Moto, Johnny Skani, HustlaJay, FikraTeule, Ohms Law Montana, Odinareh Bingwa, MamaLao, Rojo Mo,  na K Lama ni wimbo ambao ni wa Amz alioufanya 2008 alafu baadae akaifanya na mwanadada Judy Mose 2009 version zot...

Kibibi Salim Ampeleka Susumila Kortini Baada Ya Kutalakiana

Image
Kibibi Salim ambaye ni mke wa msanii Susumila amempeleka kortini msanii huyo baada ya kutalakiana na msanii huyo. Kibibi ambaye aliandikiwa talaka Septemba 4 amemfikisha msanii huyo kortini ili ahakikishe ya kwamba msanii huyo anawajibika kwa malezi ya mtoto wao Halima aka Susumilaress.   'Nilipewa talaka tatu na Susumila na nimeenda kortini ili kuhakikisha ya kwamba anashuhulikia malezi ya mwanangu. Na kingine kilichonifanya niende kortini ni kutaka eda. Katika sheria za kiislamu wanandoa wanapotalakiana, mume anafaa aendelee kuwajiba kama bwana kwa mda wa miezi mitatu kwa kua huenda watu wakaskizana na kurudiana tena.' Kibibi ameeleza. Wanandoa hao ambao tangu waingie katika ndoa wamekua wakigonga vichwa vya habari kwa sababu mbalimbali kama vile Kibibi kushtumiwa ya kwamba alimnyakua Susumila kutoka kwa mwanamke mwengine. 'Siongelei hio issue kwa sasa' ndio jibu la Susumila alilonipa nilipojaribu kumhoji kuhusu kutalakiana kwake na Kibibi ambay...