Sina Tatizo Na Susumila Wala TK2, Na Haya Ndiyo Nimepanga Kuyafanya- KIGOTO
Baada ya msanii Mswazi Masauti kuachana na management ya Swa RnB ameonekana akiwa na ukaribu sana na msanii Kigoto ambaye pia aliachana na management ya Number 1 Records ya Producer TK2 . Wawili hawa wamejitokeza na kusema kwamba wanafanya kazi pamoja ila haijabainika iwapo kushikana kwao ni kufanya collabo tu au wameunda kundi. Katika mahojiano na Kelvin Jilani (MTU BEI) , Masauti ameeleza mpangilio wao wa kufanya kazi na kile ambacho mashabiki wanapaswa kutarajia kutoka kwao. Kwa upande mwengine Kigoto naye amefunguka ya kwamba wamekua wakipata mskumo kutoka kwa mashabiki ambao wamekua wakilalamika ya kwamba wamekimya sana bila kuachia kazi yoyote kwa mda mrefu. Vilevile Kigoto ameeleza uhusiano wake na aliyekua producer na manager wake, Producer Tk2 , akijibu swali ya kipi kilichomfanya atengana na ‘mlezi’ wake huyo na iwapoo bado wanaweza kufanya kazi pamoja. Katika swali lengine ambalo lilikua limewekwa mezani na shabiki, Kigoto ameeleza maoni yake baada ya Susu...