Posts

Showing posts from December, 2015

Susumila, Sudiboy, Profesa Nasha, JayCrack, Sis P, Amz, Tee, Dazla na Dogo Richy katika video moja wakituma ujumbe wa mwaka mpya

Image
Katika Interview ya kipekee ambayo ilikua ni ya kufunga mwaka, Gates Mgenge amewafanyia interview ya pamoja  katika kipindi anachokiendesha cha  cha mashavmashavu. Baada ya interview hio Susumila, Sudiboy, Profesa Nasha, JayCrack, Sis P, Amz, Dazla na Dogo Richy wamerecord  video ya kutuma ujumbe wa Mwaka Mpya kwa ajili ya mashabiki wao. Hii hapa itazame.

Gates aanda Mombasa Allstar Interview

Image
Ikiwa leo ndio siku ya mwisho ya mwaka wa 2015, presenter wa Pwani Fm, Gates Mgenge Grandson anayeendesha kipindi cha MashaMashav ameandaa bonge la interview- Mombasa Allstar interview akiwa ameshiorikisha wasanii Sita na Producer wawili. Akishirikiana na Producer wake Lucas De Mackinon , Gates amewahost wasanii wastar hao nane kwa wakati mmoja. Walioshirikishwa katika interview hii walikua ni SudiBoy, Susumila, Dogo Richy, Profesa Nasha, Sis P, Dazlah, JayCrack na Producer Amz. Katika show hio iliyokua ni show ya kufunga mwaka mengi yamefungukwa (nitawaletea kwa mda) kuhusu kazi binafsi za kimziki lakini cha msingi wote walikua wanashukuru kwa kazi walizofanya mwaka huu, hatua walizopiga na kuwa na matumaini katika mwaka mpya wa 2016.

NEW MUSIC: Salam TMK( Mkubwa na Wanawe)-NAFSI

Image
Ni kundi kutoka kambi ya talanta ya MKUBWA NA WANAWE inayomilikiwa na Said Fella aka Mkubwa Fella yuleyule anayewalea YAMOTO BAND . Ni kundi jipya la vijana saba- OSAMA, PODO, STARBOY, ZUBERI, STAR MAPOZI, ABUUADO na FETTY na hii ndio kazi yao ya kwanza na Producer Shirko ndiye aliyetayarisha mzigo huu. DOWNLOAD/LISTEN HERE

Kundi jipya kutoka Mkubwa Na Wanawe

Image
Mkubwa Fella , ambaye ndiye mmiliki wa kituo cha talanta cha Mkubwa na Wanawe ambako ndio walikotokea Yamoto Band amezindua kundi lingine tena la vijana saba amabo ndani yao ni binti mmoja. Vijana wenyewe ni OSAMA, PODO, STARBOY, ZUBERI, STAR MAPOZI, ABUUADO na FETTY . Kulingana na Fella , kundi hilo kwa jina SALAMU TMK ni vijana anaowatoa mtaani na wanahitaji kufika mjini na kupata nguvu binafsi ya kujikimu. Kundi hili jipya tayari lina video mpya iliyoongozwa na Pablo ya wimbo mpya kwa jina NAFSI .

Wachezaji 20 bora 2015 Ligi Kuu ya Uingereza

Image
Mwaka wa 2015 ndio huu umekamili, katika Ligii Kuu ya Uingereza, timu 18 zimecheza mechi 19 isipokua Liverpool na Sunderland waliomecheza mechi 18.   bleacherreport.com ni moja wapo ya mitandao inayoandika habari na uchanganuzi wa michezo. Mtandao huu umetoa listi ya wachezaji 20 bora katika Ligi Kuu ya Uingereza mwaka huu wa 2015.  Katika listi hio kuna wachezaji wawili wa Afrika, ni ake na nani? tazama listi hio.... David De Gea (Man United/Hispania) Mesut Ozil (Arsenal/Ujerumani) Alexis Sanchez ( Arsenal/Chile) David Silva (Man City/Hispania) Sergio Aguero (Man City/Argentina) Chris Smalling (Man United/Uingereza) Santi Cazorla (Arsenal/Hispania) Harry Kane (Tottenham/Uingereza) Toby Alderweireld (Tottenham/Ubelgiji) Francis Coquelin (Arsenal/Ufaransa) Willian (Chelsea/Brazil) Riyad Mahrez (Leicester City/Algeria) Jamie Vardy (Leicester City/Uingereza) Philippe Coutinho (Liverpool/Brazil) Hector Bellerin (Arsenal/Hispania) Hugo Lloris (Tottenha...

Je CEO wa Pwani Celebrity Awards atakuwa host Wa Mseto EA?

Image
Huenda Sanita Nzaro , mwanzilishi wa Pwani Celebrity Awards akawa katika runinga yako hivi karibuni. Wakati kipindi cha Mseto EA kinachoongozwa na gwiji katika tasnia ya burudani na utangazaji, Willy M. Tuva aka Mzazi kikiwa kina kinasherehekea kutimiza vipindi zaidi ya elfu moja hapo tarehe moja Januari 2016 katika sherehe ya Mseto 1000 Live Mzazi atakua anamtambulisha Co-host wake pia. Katika watu 35 walioshiriki katika kupigania nafasi hio ya kua co-host wa Tuva, Sanita ni mmoja kati ya watatu waliobaki baaada ya mchujo. Wapinzani wa Sanita ni Yvone na  Melodi Sinzori wote wakiwa wametokea Nairobi. Katika sherehe hio ambayo itakua inapeperushwa hewani katika runinga ya Citizen Tv midaa ya saa nne kasorobo usiku, msanii kutoka hapa nyumbani SUSUMILA atakua anatuwakilisha kwani ni mmoa atakaye,perform pamoja na Nameless, Mr Nelly, Kansoul, Heat The Band, Pacho, Grandpa Team, Bahati, Denno, Jaguar, Avril na wengine wengi. 

YAMOTO Band kufunga mwaka Mombasa

Image
Katika top 10 ya nyimbo na video za mwaka East Africa nina uhakika hauwezi kukosa hawa vijana.  Kulingana na youtube, katika video 10 zilizoangaliwa sana Bongo wameorodheshwa nambari 3-nitakupwelepweta ,  5-Nisambazie raha , na pia nambari  9-Cheza kwa madoido. Ni kundi ambalo halishikika na wako on demand sana kwani wapandapo jukwaani wanatumbuiza si mchezo. Walikuwa Mombasa Mwezi wa Agosti katika uwanja wa Mombasa Sports Clubs na walitosheleza mashabiki. Watu wamekua na hamu sana ya kutaka Yamoto Band Kuja tena Mombasa . Atlast wameitikia mwito na wanaufunga mwaka Mombasa. Tarehe ni 31 Disemba. Ktika show kubwa Mombasa ya kufunga mwaka Talentos Beach Resort, Likoni ndipo watasababisha. DJ IVORY na  MC Gates Mgenge Grandson na MC TUCKER watakuwepo. Advance Tickets ni ksh.800 . Gate-ksh 1000 kabla saa mbili usiku, n KSH. 1500 baadae. Advance Tickets zinapatkana TALENTOS BEACH RESORT, 0703 725 635 na pia unaweza kulipa na MPESA. Till Number ni 550...

Ujumbe Krismasi Kutoka kwa SIS P

Image
2015 umekua mwaka wa mafanikio kwake kwani ndio mwaka aliochukuliwa na kuwekwa katika uangalizi wa A MILLION Records inayoongozwa na Producer Khalid . Si siri, A Million Records imefikisha mbali na talanta aliyo nayo kwani ameweza kufika kwa Magufuli na kufanya collabo na msanii mwenye sifa za kutajika-Barnaba katika wimbo wake wa Bonge La Bwana Remix. Sis P kwa sasa anatamba na wimbo NIRINGE NAYE Remix alioshirikiana na Alkenia na Pday. Ikiwa ndio tunaingia katika skukuu ya Krismasi, huyu hapa SIS P na ujumbe a Krismasi. BONYEZA HAPA KUMSKIA SIS P

Familia ya mwanamziki wa Injili, Annastacia Mukabwa yanusurika katika ajali

Image
Ni msimu wa Krismasi na watu wengi wako katika pilkapilka za kusafiri ili kujiunga na familia zao katika kusherehekea skukuu ya Krismasi. Asubui ya leo, midaa ya saa moja katika maeneo ya Makindu , familia ya muimbaji wa Injili, Annastacia Mukabwa imenusurika kutoka kwa ajili mbaya ya barabarani. Wakiwa wanaelekea kijijijini ambako tayari Annastacia alikua ametangulia, Mume, watoto na dereva wa gari yao binafsi walipatwa na mkosi huo. Nikiongea naye kwa njia ya simu, Annastacia alieleza ya kwamba tairi la gari lilipasuka hivyo basi kusababaisha dereva kushindwa kudhibiti gari hilo, katika ile hali ya kuepuka kugonga gari zingine barabarani, dereva amejikakamua kuelekeza gari kando ya barabara, lakini alipokanyaga brake ndipo gari lilipo bingiria mara tatu. Gari limeharibika vibaya lakini kwa bahati nzuri wote waliokuwemo katika gari hilo wamenusurika na majeraha madogo tu.

Jua iliko Studio Mpya ya Producer Amz

Image
Baada ya kujichuja kuoka kwa Studio aliyoifanyia kazi kwa miaka mitano, SQ Records, Producer Amz ametangaza sehemeu inapopatkana studio yake mpya kwa jina TEMPOZ. Wakati akiondoka SQ Records, Producer Amz alisema ya kwamba aliamua kutoka SQ Records kwani alikuua anaona mda mwafaka wa kujipanga kivyake umewadia. Aliahidi ya kwamba studio yake mpya itaanza kufanya kazi January 2016 lakini hakuwahi kusema sehemu itakayokua. Lakini hii leo, Amz ametangaza ya kwamba, Tempoz ipo njia kuu ya Mombasa-Malindi, eneo la Bamburi, kando ya Bamburi Beach , nyuma ya Kenda Bay Beach/Kahamas Hotel .

NEW MUSIC: Yamoto Band Feat Zena-MAMA

Image
Vijana wa Mkubwa Na Wanawe, YAMOTO Band wamekuja na track mpya waliyomshirikisha Zena. Inaitwa Mama . DOWNLOAD/LISTEN HERE

NEW MUSIC: Ommy Dimpoz-ACHIA BODY

Image
Baada ya kukaa kimya kwa mda, Ommy Dimpoz amevunja ukimya wake na video hii mpya ambayo audio yake ilitayarishwa na ManWater, Combination Sound. DOWNLOAD/LISTEN HERE  

NEW VIDEO: Ommy Dimpoz-ACHIA BODY

Image
Baada ya kukaa kimya kwa mda, Ommy Dimpoz amevunja ukimya wake na video hii mpya ambayo audio yake ilitayarishwa na ManWater, Combination Sound. Video hii ilitayarishwa mjini Johannesburg, Afrika Kusini na iliongozwa na OB Films .

NEW MUSIC: MB Dogg-SIO SIRI

Image
Hitamaker wa Latifa, ambaye alihit enzi zile na anayejikamua kurudi katika radar ya mziki, MB Dogg ameachia kipini kipywa kwa jina SIO SIRI. Kama kawa, hii i kuhusu mapenzi. Amejifua sana na naamini ngoma hii akiiskuma vizuri atajiweka mahali pazuri katika anga za mziki. DOWNLOAD/LISTEN HERE

NEW VIDEO: Alikiba & Christian Bella-NAGHARAMIA

Image
Ni moja kati ya ngoma kali kubwa Afrika Mashariki mwaka huu. Christian Bella ambaye mwaka huu amefanya kazi kubwa kubwa ukizingatia kua alifanya collabo na mkongwe wa Lingala, Koffi Olomide. NAGHARAMIA ni track aliyoshirikiana na mkali AliKiba na imetokea kua hit ukizingatia utulivu wa mashairi na uwezo wa sauti waliodhihirisha wawili hao katika track hio. Hii hapa ni bonge la video ya track hio, iliyoongozwa na video directro mkali toka hapa nchini, ENOS OLIK.  

Kampeni ya #PlayMyMusic ya Ng'oa Nanga hapa MOMBASA

Image
SANITA NZARO , mwanzilishi wa tuzo za Pwani Celebrity Awards akishirikiana na Wizara ya Vijana, Jinsia na Michezo, Mombasa County ameanzisha kampeni ya #PlayMyMusic . Kampeni hii ni ya kupigania na kuhakikisha ya kwamba asilimia 60 ya mziki unaochezwa katika maeneno ya burudani ni mziki kutoka Mombasa. Hii ni kujaribu kuwezesha wasanii waweze kupata kipato kupitia royalties na wasanii kupata exposure vizuri kwa mashabik. Kampeni hio ambayo ilianzishwa rasmi na waziri wa vijana, jinsia na michezo Mheshimiwa Mohammed Abbas hapo jana katika Pwani Showcase Night iliyofanyika Bliss Resort. Akiongea katika uzinduzi huo, Mheshimiwa Abbas alisema kwamba hivi karibuni sana, watakua na mkutano na wamiliki wa maeneo ya burudani ili kupanga mikakati hio itakayowezesha  lengo la kampeni hio kufanikishwa. Vilevile, aliahidi ya kwamba kutakuwepo na sheria katika kaunti ya Mombasa kusisitiza na kuhimizia ya kwamba mziki unaochezwa katika maeneo ya burudani iwe asilimia 60 . Sanita ali...

Photos From Pwani Showcase Night

Image