Posts

Showing posts from November, 2015

NEW MUSIC: Wawindaji-JANJA

Image
Ni chipukizi wawili mandugu ambao wali,hit sana na album yao enzi zile Dj Badaga akiingia katika industry. Mara kidogo wakaenda kimya, na hivi sasa waweamua kurudi tena na style mpya. Ni kama vile walikua wako jikoni wanapikwa kwani track hii wameweza na inadhihirisha hawakua wamekimywa kwa kuishiwa na utunzi bali walikua wanajipanga kuja na style mpya na ujio mpya. Bonyeza hapa ku,download/kuskiliza

NEW VIDEO: Matonya-HOMA YA JIJI

Image
Mkongwe wa bongofleva, hitmaker wa vaileti, Matonya ambaye yuko mbioni kuchukua nafasi aliyokua akishikilia enzi zile baada ya kuoa track mpya mwisho wa wiki jana ameachia hii vdeo mpya ya wimbo HOMA YA JIJI. Ni video ilioongozwa n Tonee Blaze  

Dogo Richy Katika Scandle Nyengine

Image
Ikawa ni siku ya Jumamosi na kila msanii anayefaya vizuri kwenye mziki wikendi zinampata katika mishe za matamasha. Siku ya Jumamosi iliyopita Dogo Richy msanii anayefanya vizuri na kibao cha yoyobah alihitajika kupiga show katika klabu ya kalahari iliyoko maeneo ya watamu show ambayo richie alikua amelipwa tayari down payment.Chakushangaza Richy Ree alifika maeneo lakini ilipofika mda wa kupanda stage jamaa hakuonekana hali ambayo iliwafanya wadau walioandaa show hiyo kupaniki na mwishowe ikawabidi waregeshe hela kwa mashabiki ambao tayari walikua washalipia show... Je kipi kilichopelekea Richy Ree kuipiga chini show hiyo? Tulifanikiwa kupanda pande zote mbili ikiwa ni umiliki wa klabu ya Kalahari pamoja na Dogo Richy mwenyewe na kila mmoja alikua na data za kujitetea skuliza pande zote mbili zikijieleza

Mtangazaji wa Baraka F.M,Nelly Mwikamba apata pigo

Image
Hapo jana, mtangazaji  wa Baraka F.M ambaye amewahi kushinda tuzo mbili Nelly Mwikamba alipata pigo. Mume wa Nelly Mwikamba alihusika katika ajali mbaya ya barabara wakati akiendesha gari. Bwanake Nelly aligonga gari nyeupe aina ya Harrier maeneo ya Shanzu katika  barabara kuu ya Mombasa-Malindi . Katika ajali hio, alivunjika mfupa wa paja mara mbili na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji  baadae hii leo.Upasuaji huo unatarajiwa kugharimu takribani shilingi Laki Tano . Nelly ambaye ni hivi majuzi tu alijaaliwa mtoto huendesha kipindi cha jioni kwa jina ON THE LANE akishirikiana na Captain Lui. Pia ni mmoja wa walioteuliwa kuwania Mtangazaji Bora wa Kike katika tuzo za Nzumari zitakazofanyika tarehe 11 mwezi wa Disemba katika hoteli ya kifahari ya Flamingo Beach -kutoka kwa meza yetu ya habari tunamtaki bwanake Nelly afueni ya haraka

NEW MUSIC: Matonya-JELA KIDOGO

Image
Hii hapa ni track mpya ya mkongwe na mkali wa mziki wa bongofleva Matonya aka Tonyatym ambaye anang'ang'ana kurudi kwenye nafasi ya juu aliyokua enzi zile aki,hit na track kama Vaileti na Anita. bonyeza Hapa kui,download/kuskiliza  

NEW VIDEO: Kassim Mganga Feta Christine Bella-SUBIRA

Image
Baada ya takriban miezi tisa tangu wimbo Kassim Mganga aka Tajiri wa Mahaba kuachia wimbo wake aliomshirikisha Christine Bella hatimaye video ya hit hio imedondoshwa. Ni video iliyotayarishwa na Adam Juma . Location nzuri za ufuoni na wametumia wanenguaji wanaoweza kazi yao.

KideKide yateuliwa katika Tuzo za Pulse Music Video Awards

Image
Kilicho na sifa kipewe sifa na kazi nzuri siku zote haifichiki kwani kwa kila kila njia hua itajiuza tu. KideKide ya Dazlah aliyomshirikisha Susumila ni track ambayo imetamba sana katika anga za mziki na kwa takriban miezi saba saa hii, ndiyo wimbo kutoka pwani unaoongoza kwa kuchezwa sana. Hit hii ambayo ilitayarishwa na Producer Tee wa Tee Hits na video ya wimbo huu ambayoo ndio imeteuliwa iliongozwa na kutayarishwa na Hamza Omar wa ONE MONTAGE FILMS imeweza kuteuliwa katika tuzo za PULSE MUSIC VIDEO AWARDS katika kitengo cha BREAKTHROUGH VIDEO OF THE YEAR.   Katika tuzo hizo zenye vitengo 10,  KideKide ndio wimbo wa pekee kutoka pwani. Ushindi wa Dazlah na Susumila na sanaa ya pwani kwa ujumla iko mikononi mwako kwani mshindi anabainiwa kwa wingi wa kura zitakazopigwa na mashabiki.Tuwe wazalendo na kwa pamoja tuweze kuwapa Dazla na Susumila uwezo wa kunyakua tuzo hii kwa kutuma ujumbe mfupi wa neno PMWA8a na utume kwa 22845 , KWA GARAMA YA SHILINGI MOJA ...

NEW VIDEO: Mswazi Masauti-MAHABUBA

Image
Zile ngojangoja sasa kwishney. .....ile video ya mkali wa utunzi aliyejaaliwa sauti kama jina lake linavyoashiri, Mswazi Masauti imedondoshwa uraiani. Ikiwa hii ndio kazi ya kwanza chini ya ulezi wa producer mkongwe nchini, Ted Josiah wa SwaRnB Records, bila shaka Masauti amegonga ndipo kwani hii ni track kali sana na video imefunika ile mbaiya.

Mswazi Masauti afafanua kwa kina ujio wake na hali yake kimziki

Image
Mswazi Masauti ni msanii mwenye ambaye amejaaliwa kipaji cha utunzi na sauti si haba ametamba kwa track kama vile Uko Wapi, Siwezi, Usikate Tamaa na Niko Nawe ambayo aliifanywa wakiwa kundi la Number One Academia [SudiBoy, Chapatizo, Kigoto, Masauti]. Baada ya kutoa wimbo wa Niko Nawe akiwa Number One Academia amekua kimya sana, je kulikono? Kuna changamoto zinazomnuweka kimya? kama zipo, ni gani.... Bado yupo Number One Academia ? Mashabiki wake wasubirie kitu gani? Huyu hapa Masauti akizungumzia kwa kina kuhusu hali halisi ya kazi zake za mziki bonyeza hapa kumskiliza MASAUTI

NEW MUSIC: Rich Mavoko-NAIMANI

Image
Baada ya kushirikishwa katika nyimbo nyingi katika siku za hivi karibuni, Rich Mavoko hatimaye ameachia hii yake mpya kwa jina NAIMANI. Bonyeza Hapa K,skiliza/ku,Download  

Producer Amz afunguka kwa undani sababu za yeye kutoka SQ Records

Image
Baada ya Producer Am z kutangaza kujiuzulu kama producer wa SQ Records na kuasema kwamba anajipanga kuja upya na studio yake ifikapo Januari 2016 , mengi yamesemwa kama vile ya kwamba hakujiuzulu ila amefutwa kazi. Haya hapa ni mhojiano na AMZ akieleze kuhusu tetesi za kwamba alifutwa kazi. Na vipi swala la kua hard disk zilipotea na kazi zote za wasanii ambazo zilikua hazijatoka kupotea? Kulikua na ugomvi wowote au kutoelewana kati ya producer Amz na Steve ambaye ndio mmiliki wa SQ Records ? BONYEZA HAPA KUSKILIZA MAHOJIANAO HAYO

Producer Amz aondoka SQ Records

Image
Producer wa hits kama vile Tuliza Nyavu, Chanda Chema, My Voice My Choice , Producer Amz ametangaza kutoka rasmi katika studio za SQ . Ikiwa hii leo ndio ambayo Amz anakamilisha miaka mitano kuhudumu kama producer wa SQ Records , ndio siku ambayo AMZ amejitoa rasmi katika studio hio. Sq Records ilifunguliwa mwaka wa 2008 na ma,producer waliotangulia kufanya kazi SQ ni V-Sita, TK2 , Shirko na Kroniqs . Hio inamaana Amz ndiye producer aliyedumu kwa mda mrefu ndani ya SQ Records. Kupitia kwa njia ya simu Amz ameeleza ya kwamba ameamua kutoka SQ na anajipanga kuja na stuio yake kwa jina TEMPOZ ambaye itaanza kazi rasmi Januari 2016. Vipi kuhusu kazi alizokua anazishuhulikia? "kwa sasa kazi hizo hazipo, Steve (mmiliki wa SQ Records ) alianiambia ya kwamba harddisk ziliibiwa wakati studio ilipokua inafanyiwa ukarabati".... AMZ alieleza

Jamaa ajinyakulia dola 500 katika shindano la mwanamme mwenye sura mbaya zaidi

Image
Kuna mashindano mengi duniani, kama vile ya urembo, mvuto, kupendeza ila pia usishangae kwa hili kwani pia nchini Zimbabwe kuna mashindano ya mtu mwenye sura mbaya zaidi. Maison Sere , ambaye hana meno kadhaa mdomoni aliwapiku washindani wengine watano na kukwarua mkwanja mrefu kiulaaiiiiiini. Jombi huyu mwenye umri wa miaka 42 aliyeibuka mshindi katika shindano hili la kua na sura mbaya zaidi  hana kibarua alituzwa kitita cha dola 500 kwa kua na sura mbaya zaidi. Kama kawaida, katika kila shindano, hakukosi malalamiko haswa washindani wasiokubali kushinwa na shindano hili pia lilipata malalmiko kutoka kwa mshindani William Masvinu ambaye amewahi kushinda shindano hilo mara tatu mtawalia alilalamika na kusema kwamba mshindi Miason alipendelewa ndiposa yeye akaibuka wapili lakini yeye ndiye aliyestahili tuzo hio. Shindani hilo limegonga vichwa vya habari na hii hapa ripoti kutoka kwa kitua cha CCTV, China  

kionjo cha video mpya ya Mswazi Masauti-MAHABUBA

Image
Ikiwa ndio project ya kwanza tangu aingine katika uangalizi wa producer mkongwe nchini, Ted Josiah , kijana wa nyumbani mwenye uwezo, talanta na juhudi za kufa mtu Mswazi Masauti anatarajiwa kuangusha bonge la track pamoja na video yake siku ya Ijumaa, 27 Novemba 2015 . Mashabiki na washika dau wakiwa katika mkao wa kula kutaka kujua ni kipi Masauti atatuangushia kutoka kwa SwaRnB records , chini ya uongozi wa Ted Josiah, hiki hapa kionjo cha kazi hio inayosubiriwa kwa hamu na ghamu

Susumila na Kush Tracey kurudia Video ya wimbo UMENITOSHA

Image
Video ya msanii SUSUMILA akimshirikisha mwanadada  KUSH TRACEY ni moja kati ya zile projects ambazo zimesubiriwa sana na mashabiki wengi  wa mziki kwa sasa. Ukizingatia kuwa ni moja kati ya kazi ambazo zilipigiwa debe sana huku picha za utayarishaji wake zikitawala mitandaoni. Ni dhahiri kwamba subira ya wengi imefikia kikomo na uvumilivu wa wengi umeanza kutibuka. Kwa wengi walio na maswali kuhusu video ya wimbo huu wanafaa kujua kuanzia leo kuwa baadhi ya vipande vya video hiyo havikutokea ilivyotakikana kwa hivyo video hiyo inapangwa kurudiwa tena ili kurekebisha makosa yaliyokuwepo.  Mbali na video ya umenitosha,  msanii SUSUMILA alikua ameahidi ngoma kadhaa ikiwemo video ya wimbo aliyoshirikishwa na  Dazlah , Bangereba Rmx. Tukisubiriavideo rasmi ya wimbo huo, kunayo video yake ya animation iliyotayarishwa na Rikky Bekko ikiwa ndio video ya kwanza ya mtindo wa animation kuwahi kufanyiwa msanii wa Pwani.

NEW MUSIC: Dogo Dee Feat Baraka Da Prince-WABANA RIZKI

Image
Rapper mwenye umri mdogo kabisa mwenye umri wa miaka 14 katika mziki wa Tanzania, Dogo Dee ameshirikisha mwimbaji mwenye sauti na utunzi, Baraka Da Prince katika kipini hiki kipya kwa jina Wabana Rizki CLICK HERE TO DOWNLOAD/LISTEN  

NEW MUSIC: Nas Junior Feat Mr.Blue-MLETE

Image
Nas Junior amemshirikisha hitmaker Mr.Blue katika track hii ya hiphop kwa jina Mlete . Ni track kali sana, chukua mda wako kuiskiliza/kui,download.   CLICK HERE TO LISTEN/DOWNLOAD

NEW MUSIC: Dully Sykes Feat Yamoto Band-TUACHIE

Image
Mkongwe wa bongo fleva, Prince Dully Sykes aka Mr. Misifa aka Brazameni amewashirikisha vijana wanaotamba katika mziki wa Africa Mashariki-Yamoto Band katika hii inaoenda kwa jina TUACHIE. SIKILIZA HAPA  

MZIKI WA SIKU HIZI HAUNA UNDERGROUND WALA MKONGWE, WOTE SAWA

Image
Muziki wa siku hizi hauna cha mkongwe wala underground, kama huamini uliza wakongwe flani ambao kwa sasa wanatapa kufa maji. Msanii kujiita underground ni kujidharau mwenyewe. Kinachotofautisha wasanii siku hizi ni bidii na kipaji na sio ukongwe na umaarufu. Kama wasemavyo wahenga kuwa mtaji wa maskini ni nguvu zake , naona pia mtaji wa msanii yoyote ni kipaji na bidii yake. Zamani kidogo miaka flani ya nyuma kupenya na kuitawala sanaa ilikua rahisi saana kwa sababu ya ufinyu wa ushindani uliokuwepo. Miaka hiyo ambapo sanaa ndio ilikua inajitengenezea jiwe la msingi, msanii alikua anaweza kuimba kitu chochote na watu wakamkubali. Miaka hiyo pia ni wakati ambapo msanii alikua anaweza kutawala chati na wimbo mmoja kwa takriban miaka mitatu akipiga shows na kubaki gumzo kwa midomo ya wengi kwa kipindi kirefu. Hukuhitajika kama msanii kuwekeza pesa nyingi kwa video za ubora kama ilivyo sasa ili ufanye vizuri.Wakati huo pia katika vipindi vingi vya redio hakukua na ushindani mkubwa vil...

NEW VIDEO: Wasojali Band-NAHISI UCHUNGU

Image
Vijana wanaoteja anga za mziki na ambao bado video yao ya Jirani waliyomshirikisha Susumila inatamba, wamekuja tena na video mpya ya wimbo wao #NAHISI_UCHUNGU.  

NEW MUSIC: Nay WaMitego-NYUMBANI KWETU

Image
Nay WaMitego ni msanii ambaye amejaaliwa na talanta si mchezo. Akiimba shwari, aki,rap anafunika. Ni mmoja ya wasanii ambao huezi sema ni rapper au muimbaji kwani pande zote mbili anaweza. Kama umekua ukimfuatilia utaweza kuona anatoa nyimbo moja ya hiphop alafu inayofuata ni kuimba. Sina Mda ndio wimbo wa mwisho alioachia na sasa amekuja na #Kwetu_Nyumbani, track amabyo ameimba kwa style ya mduara.   BONYEZA HAPA KUSKILIZA/KUPAKUA

Daddy Selle amekua wapi? Amewacha mziki? Ataachia wimbo mpya Lini? Msikilize

Image
Ni msanii aliyetamba saana na kibao cha #Machungu na #Ananipenda miongoni mwa vingi vilivyotawala chrt za mziki kwa siku nyingi. Wengi wamekua wakijiuliza jamaa kaenda wapi baada ya kimya kirefu. Tumemtafuta Daddy Selle ili aweke wazi majibu ya maswali ya wengi..... Je, amewacha muziki? na kama amewacha anafanya kazi gani kwa sasa? Na kama hajawacha mziki ni lini mashabiki wake wanafaa kutarajia kitu kipya kutoka kwake? Bonyeza link kusikiliza alichokisema Daddy Selle mwenyewe kuhusu safari yake ya mziki.... mskilize Daddy Sele HAPA  

NZUMARI AWARDS 2015 Nomination List & Voting Platform Link

Image
  Tuzo za kila mwaka za NZUMARI AWARDS KENYA zimepangwa kufanyika siku ya Ijumaa 11 Disemba 2015 katika hoteli ya FLAMINGO BEACH RESORT. Wateuliwa wa kila kitengo ni kama ifuatavyo.. MALE ARTISTE MOMBASA Dazlah Amour Beybe Sudi Boy Brown Mauzo Dogo Richee     MALE ARTISTE TANZANIA AY Ali Kiba Ommy Dimpoz Shetta Rich Mavoko     MALE ARTISTE NAIROBI Jaguar King Kaka Khaligraph Jones Octopizzo Kenrazy     FEMALE ARTISTE MOMBASA Love Mumz Vivonce Sis P Mama Lao Jovial     FEMALE ARTISTE TANZANIA Shilole Linah Vanessa Mdee Lady Jay D Shaa     FEMALE ARTISTE NAIROBI Avril Victoria Kimani Amileena Size 8 Wahu     ARTISTE OF THE YEAR MOMBASA Ali B Chikuze...