Posts

Showing posts from December, 2016

Skiza Alichokifanya Msanii Huyu Baada Ya Kuachwa Na Mpenzi Wake

Image
 + Wanasema hakuna kitu kizuri zaidi ya kupendwa na pia hakuna maumivu zaidi ya kutemwa na unayempenda. Hayo maumivu yatakuzidi endapo unayempenda atakuacha, si kisa pesa wala kwa kua amepata mpenzi mwengine...nooo, kisa kajiskia tu. Ndio yaliyomkuta msanii Agalanta ambaye aliachwa na mpenzi wake wa mda mrefu bila sababu tu. Kwa uchungu aliyokua nao ikabidi aingie studio na producer wake Swahib Wa Maselle wafanye wimbo wa MAUMIVU ambao alitiririka hisia zake >> HAPA

Producer Khalid Atiwa Mbaroni

Image
Baada ya vuta nikuvute ya siku mbili kati ya msanii PDay na Producer Khalid, drama kati ya wawili hao haijaishia mtandaoni tu bali imesababisha Producer Khalid kutupwa korokoroni. Malumbano yote hayo yalianza hapo jana wakati PDay aliandika katika katika ukurasa wake wa facebook ya kwamba Producer Khalid amedinda kumpatia video aliyomtayarishia akidai ya kwamba mabinti waliotumika na msanii huyo katika video hio ni wabovu. Wakati Khalid akijibu madai hayo, alisema ya kwamba msanii huyo ni mtu asiyekua na shukrani. Pday naye amemgeuzia kibao producer huyo akisema ya kwamba Khalid ndiye wa kwanza kukosa shukrani kwani hata yeye ndiye aliyemsaidia kupata loan yake ya kwanza kwa 'mzee Rajab'. Kufikia mida ya saa kumi na robo alasiri, kumeanza kuenea uvumi ya kwamba producer Khalid ametiwa mbaroni, ili kuthibithisha uvumi huo, Gates Mgenge katika kipindi cha MwakeMwake, PiliPili Fm amempigia simu PDay ambaye ameeleza yaliyojiri... 'Khalid ni kakangu wa mda mrefu...

PDay Na Producer Khalid Wafunguka Kuhusu Khalid Kukataa Kutoa Video Ya PDay Kisa Madem Wabovu

Image
‘…Wale mademu uliolea walikua wabovu kwa hivyo tafta wengine na venue nyingine tu,shoot tena…’ ni  kipande cha post ambayo Pday alipost katika mtandao wa facebook akidai ya kwamba Producer Khalid wa A Miliion Records/Vision amemdhulumu pesa zake baada ya ku,shoot video alafu baadae akamgeuzia lugha na kudai ya kwamba vixen waaliotumiwa walikua wabomu kwa hivyo video inafaa kurudiwa tena. PDay ambaye anaonekana mwingi wa hasira amefunguka kwa kina kuhusu madai hayo ya kutapeliwa na Producer Khalid kwa kueleza mpangilio wao wa kazi hio ulikuaje kuanzia mwanzo hadi sasa kufikia kudaiana mitandaoni katika mahojiano yake na Kelvin Jilani/Mtu Bei   >>   HAPA Khalid naye ambaye amedai ya kwamba Pday ni mtu asiyekua na shukrani na anatafuta kiki na pengine ametamani kupata likes na comments za facebook  ndio maana anafanya anayofanya.  ‘Ni kweli alileta mademu ambao wamechoka lakini hio si sababu ya mimi kuzuia video yake, nilikua nampa ushauri tu...

Chikuzee Na Susumila Waelezea Uhusiano Wao Baada Ya Kupiga Show Pamoja

Image
  Combination ya wasanii hawa wawili wakubwa ni combination ambayo hua imekubalika sana. Track zote mbili ambazo walizifanya pamoja zilitokea kua hits. Urafiki wao ulikua wa mda kwani baadae walianza kua na tofauti wakati ambao hata mashbiki walikua wanatamani wawili hawa waunde kundi. Siku ya ' Boxing Day ' wawili hao wali,surprise mashabiki mjini Malindi baada ya ku,perform pamoja nyimbo zao mbili. Ni jambo ambalo liliweza kusisimua hisia za mashabiki na washikadau mbalimbali katika sanaa ya mziki. Je ilikuaje mpaka wakapanda jukwaani kwa pamoja? Hivi ina maana wawili hawa wametupilia mbali tofauti zao? Je ile kiu ya mashabiki ya kutamani kazi nyengine ya pamoja kutoka kwa wwili hawa huenda ikatoshelezwa? Wasanii hawo wawili waliweza kuzungumza kwa kina na Kelvin Jilani /Mtu Bei na kuweza kufungua kwa kina kuhusu maswali haya katika mahojiano yao >> HAPA

Queen Renee Awazawadia Mashabiki Zawadi Ya Kufunga Mwaka

Image
Umekua mwaka wa kazi kwa msanii Queen Renee. Baada ya kumaliza tour yake ya miezi minne mwishoni mwa 2015 nchini Ujerumani, Italy na Switzerland , alirudi nchini na ku,launch album yake ya CHAMPAGNE . Ni album ambayo imebeba nyimbo 12 na huu mwaka ameachia nyimbo tano kutoka kwa album hii. Ikiwa ndio wiki ya mwisho ya mwaka, Queen Renee ameamua kuwazawadia mashabiki wake video mpya ambayo ndio atakua anafunga nayo mwaka.

Orodha Kamili Ya Washindi Wa Kenya Coast Music Awards 2016

Image
Tuzo za Kenya Coast Music Awards 2016 zilifanyika usiku wa Jumamosi, Disemba17. Walioibuka Washindi nii.... (1). DANCE GROUP OF THE YEAR -TSUNAMI (2). PROMISING ARTIST OF THE YEAR - JAFARIZZO (3). BLOGGER OF THE YEAR - MACHAMPALI (4). GOSPEL SONG OF THE YEAR -  MWEMA-Mercy Masika (5). COLLABORATION OF THE YEAR -  NITALIA NAWE- Wasojali ft Kalechi (6). GROUP OF THE YEAR  WASOJALI (7). BEST FEMALE ARTIST OF THE YEAR  Jovial (8). BEST MALE ARTIST OF THE YEAR  Sudi Boy (9). DIASPORA ARTIST OF THE YEAR  Cannibal (10). EAST AFRICAN ARTIST OF THE YEAR  King Kaka (11). BEST AUDIO PRODUCER OF THE YEAR -  Totti (12). BEST ACTRESS OF THE YEAR -  Kibibi Salim (13). BEST ACTOR OF THE YEAR -  Juma Shibe (14). FREELANCER DJ OF THE YEAR -  DJ Cypee (15). CLUB DJ OF THE YEAR -  DJ Maps- Sheba Lounge (16). FEMALE DJ OF THE YEAR - DJ Russian- Club Hypnotica (17). NIGHT SPORTS CLUB OF...

Susumila Ampoteza Babake

Image
Hitmaker wa Tuliza Nyavu , msanii Susumila ambaye alimpoteza mamake mzazi mnamo 2014 amepata pigo tena kwa kumpoteza babake mzazi. Mzee Kombo Kinando Tangai ambaye ni mkaazi wa C humani alikua na umri wa takriban miaka 70. Akinieleza habari hizo, Susumila ameeleza ya kwamba mzee Kombo aliugua kwa mda mrefu kabla ya kuaga dunia asubui ya leo. ' Mzee ametuacha asubui ya leo. Bado tunaendelea na mipango ya mazishi lakini kuna uwezekano mkubwa ya kwamba tutampumzisha Jumamosi hii ya tarehe 24 nyumbani Chumani. ' Susumila amesema. Tuna wapa pole familia ya marehemu Mzee Kombo , Mungu awajaalie wepesi katika wakati huu mgumu na ampumzishe mwenda zake kwa amani.

Matonya Ataja Wasanii Watatu Kutoka Mombasa Ambao Anawakubali Sana

Image
Matonya ni mkongwe  wa bongofleva  ambaye alianza  kushika  anga za mziki  katika miaka ya 2005  na wimbo wake wa Vaileti . Ni zaidi ya miaka kumi sasa tangu aanze kupenya anga za juu za mziki na, style zinaenda zikibadilika na  jinsi ya kufanya mziki kubadilika lakini ameweza ku,maintain na kurudi tena katika chati za mziki na kuweza kushindana tena na wanamziki ambao wameibuka  na ari na mbinu mpya. Matonya ambaye yupo mjini Mombasa alifunguka katika mahojiano yake na blog hii kuhusu siri iliyomuwezesha kuduma  katika game   na  kuweza kurudi  tena baada ya  kukaa kimya kwa mda. Vile vile Matonya amewataja wasanii watatu ambao anawakubali kutoka eneo la pwani. 'Kusema ukweli wasanii ni wengi sana lakini kuna huyu msanii anaitwa Susumila namkubali sana. Pia Chikuzee nampenda sana. Paneli pia ni msanii ambaye namkubali na tayari niko na collabo naye na ntakua nashoot video naye wikendi hii. Ila Susumila na Ch...

Mziki Ulimshinda Kwa Kukosa Pesa, Lakini Sasa........

Image
Mmoja kati ya wasanii ambao wanainukia vizuri katika tasnia ya mziki wa kizazi kipya ni msanii Chabush Izo . Japo kua hajaskika sana ila si mgeni sana katika sanaa ya mziki kwani tayari ashafanya kazi katika studio tajika mjini Nairobi , kama vile Homeboys Records na Alpha Records ambako alifanya track kama vile Mimi Nakupenda, Maisha Noma na baadae ' Digital' ambayo alimshirikisha Aim Jeezy . Ni miaka miwili sasa tangu aache mziki baada ya kuona ya kwamba alikua anafanya mziki na anakosa support haswaa ya kifedha ukizingatia ya kwamba soko linahitaji kazi zenye ubora na huwezi tayarisha kazi za ubora bila hela nzuri. Changamoto hio ndio iliyomfanya asitishe mziki wake ili aendeleze taaluma yake  ambayo ameisomea. 'Mda wote nliokua kimya nilikua najenga career yangu ambayo nimeisomea na kwa sasa nashkuru kwasababu nimepiga hatua nzuri na pia nimeanzisha biashara zangu na ni juzi tu nimeweza kununua gari. Kwa sasa nategemea changamoto zingine si kama zile za kwanz...

GreenHouse Records Yatambulisha Msanii Mpya

Image
Moja ya studio za mziki ambazo zimedumu sana mjini Mombasa ni studio za GreenHouse Records . Ni studio ambayo imezalisha na kukuza wasanii wengi tajika katika sanaa ya mziki happa pwani. Wasanii kama vile Susumila, Kidis, Nyota Ndogo, Chapatizo, Escobar ni baadhi ya wasanii tajika ambao wamepitia katika mikono ya studio hio ambayo kwa sasa ina wasanii wapya ambao wameanza kuteka nyoyo za wengi kama vile Wasojali Band, Kelechi Africana na Dizzle Leo. Studio hio ambayo imekua ikionyesha kulea vipaji kwa kiasi kikubwa  chini ya producer wa sasa Noizer wametambulisha tena msanii mpya kwa jina Stiv Adamz ambaye tayari ameachia track mpya kali kwa jina EVERYBODY DANCE ambayo unaweza kuipata >> HAPA

Mpenzi Mpya Wa SudiBoy Azungumzia Wimbo Wa SudiBoy Mpya Ambao Unaongelea Kuhusu Past Yake

Image
Anaitwa Kashata, baiby baiby wa Sudiboy amefunguka na kusema kwamba yeye ndio alimskuma Sudiboy autoe wimbo wake wa "Kidonda" ambao unabeba ujumbe mzito kumhusu marehemu mkewe. Kulingana na Kashata ni kwamba Sudiboy alikua asharekodi wimbo huwo ila alikua anaghairi kuutoa huku akiwa bado anaonekana kupitia wakati mgumu wa kumpoteza mkewe mpendwa. Kulingana na Kashata ni kwamba wimbo huo ni kama mwanzo wa safari mpya wa Sudiboy huku akimtabiria makubwa chini ya management mpya aliyonayo kwa sasa. 'Unajua kila mtu ana past yake. He had the song but hakua anataka kuutoa but i told him, akiutoa ndio atakua relieved .'' Kashata aliyasema hayo katika mahojiano yake na Kelvin Jilani / Mtu Bei huku akiendelea kufunguza zaidi jinsi alivyochangia kuachiwa kwa wimbo huo na stori ya wimbo huo. Pata kuskiliza mazungumzo hayo >> HAPA

Matonya Kufanya Haya Mjini Malindi Wikendi Hii

Image
Matonya ni msanii ambaye alihit sana miaka ya nyuma kidogo. Japo kwa sasa bado hajashika kasi sana lakini bado anatoa mziki mzuri na zile nyimbo zake za kitambo tu bado zinapendwa kwa sana kwa style ya mziki wake ni tofauti na wa sasa ambao hua una,hit kwa miezi kidogo tu na kupotea, ndio maana hata wengine huuita 'bubblegum music '. Wikendi hii, akiwa na msanii kutoka Mombasa, Paneli ambaye amehamisha makao yake nchini Italy ila ailitua nchini wikendi iliyopita atakua ana,shoot video ya collabo yao mjini Malindi .Video hio ya wimbo TEMPARATURE , itakua inaandaliwa kiaina chini ya uongozajiwa wa director maarufu, Johnson Kyalo ambaye ametayarisha video kama vile Mapepe ya Susumila na KingKaka na video zengine nyingi. Utayarishaji wa video hio utakua unafanyika katika tamasha event ambayo Matonya , Paneli na Lil Mizee watakua anatumbuiza katika ukumbi wa WATAMU CLUB , usiku wa Disemba 17 na kiingilio itakua Kshs.300 tu!!

Orodha Kamili Ya Washindi Wa STYLUS DJs AWARDS 2016

Image
Toleo la 4 la tuzo za Stylus Djs Awards lilifanyika wikendi iliyoita katika ukumbi wa Mamba Village, Nyali. Katika sherehe hio ambayo  Mc's wa siku walikua  Presenter Dee aka Presenter 001 wa Baraka FM   na Chapatizo na performances kutoka kwa Frankie Dee, Kitole Kenda, Romrommy, Wasojali Band, Ohms Law Montana, Ramesh, Jovial, SisP, na XAV Gang   walioibuka  washindi  ni..... 1. BREAKTHROUGH DJ OF THE YEAR Dj Koks – Kwale County 2. CLUB DJ OF THE YEAR (MOMBASA)  Dj Geeps 254 – Dan’s Lounge 3. CLUB DJ OF THE YEAR (NAIROBI) Dj K-Rich – Tribeka Restaurant & Pub, Banda Street 4. REGGAE DJ OF THE YEAR DJ BUNDUKI 5. RHUMBA DJ OF THE YEAR DJ 2ONE2 6. EDM DJ OF THE YEAR DJ PROTÉGÉ 7. GOSPEL DJ OF THE YEAR DJ GEEGEE 8. RADIO DJ OF THE YEAR (NAIROBI) DJ CHRIS STYLUS – MILELE FM 9. RADIO DJ OF THE YEAR (MOMBASA) VJ ACE – BAHARI FM 10. TV VJ OF THE YEAR DJ ANDIE – KBC 11. FREELANCE DJ OF THE YEAR (TRAIL BLAZER DJ) DJ JO...

MC Kimbo Ni Msanii Mkubwa Sana Na Hafai Kuishi Anavyoishi, Aeleza Timmy T Dat

Image
Timmy T Dat ndio msanii ambaye kwa sasa ni 'hotcake' nchini Kenya. Ni msanii ambaye nyimbo zake kwa sasa zinahit na anapiga show nyingi za pesa ndefu. Tarehe mbili mwezi huu, alikua na show mjini Kilifi na kulingana na yeye, kama kawaida yake hua akifika 'mashinani' hua anafanya research na  kujaribu kujua wasanii ambao wanashika   na wanaweza katika eneo hilo. Siku ya uzinduzi wa video mpya ya SudiBoy, Pascal Shanga wa kipindi cha Chachawiza, Bahari FM alikutana na Timmy katika launch ya video KIDONDA ya SudiBoy . Timmy alifunguka jinsi alivyoona uwezo mkubwa wa mziki alionao Kimbo lakini kile kinachomhuzunisha ni kwamba msanii huyo anaishi maisha ambayo hayapendezi kabisa. 'Nilisifiwa sana kwamba Kilifi kuna msanii anaitwa Kimbo na nkafanya bidii nkaonana naye sku iliyofuata. Kimbo ni star, hafai kuishi vile anavyoishi. Kusema kweli nilipenda uwezo wake na kuna kitu kitafanyika...sitasema kwa sasa but watch this space .' Timmy alisema. Sikiliza m...

DJ Lenium Afunga Harusi Tena (Photos)

Image
Amekua katika sanaa ya mziki kwa takriban miaka kumi na tatu sasa na anajivunia kuwa na tuzo kumi kutoka kwa kazi zake tofauti anazofanya katika tasnia ya burudani ikiwa uigizaji, ku,mc, utangazaji, na u,DJ. Ikiwa leo ni siku ya 9, Disemba , mkongwe huyu katika sanaa ya burudani katika eneo la pwani amefanya sherehe ya kuadhimisha miaka mitano tangu afunge pingu za maisha na mkewe, Maureen Angira ambaye wamejaaliwa watoto wawili pamoja.   Sherehe hio ambayo imefanyika katika kanisa ya St Stephens ACK Bamburi , ilihudhuriwa na marafiki kidogo sana na familia. 'Si rahisi kuona mtu ambaye yuko katika sanaa, haswa dj kudumu sana katika ndoa. Nashkuru sana kufikisha miaka mitano katika ndoa na ndio maana nikachukua ya ku,renew vows tena kanisani kwa kua nachukulia serious ndoa yangu na familia yangu.' Dj huyo ameeleza huku akionyesha wingi wa furaha.   Kutoka Machampali Media, tunamtakia DJ Lenium na Maureen amani katika ndoa yao na iendelee kudumu. Hizi hapa ni baa...

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele

Image
Ukitaja wasanii ambao waliwahi kutamba kutoka eneo la pwani huwezi kukosa kumtaja Daddy Sele . Miaka ile ya 2008 alikua anatamba sana na wimbo wake wa Machungu na Ananipenda , wimbo ambao aliufanya na Fat S .  Wimbo wake wa Machungu , uliotayarishwa BC International ndio single yake kubwa ambayo ilimfanya atese sana katika anga za mziki baada ya kufanya track kama vile Badman , aliyokua ameifanya katika studio za Tabasamu Records ambayo haikuwahi kupata airplay nzuri. Kwa sasa, Daddy Sele ameacha kabisa mziki na kulingana na yeye ni kwamba yeye kufanya mziki basi itakua ni miujiza, aliongelea hilo >> HAPA. Kila siku ya alhamisi utakua unapata fursa ya kupata wimbo/video moja ya kitamboooo... unaweza ku,request katika eneo la ku,comment hapo chini. Download/Listen MACHUNGU >> HAPA

Kurushiana Makonde Kati Ya Susumila Na Wazo Baba Kwasitisha Shoot Ya Video Yao

Image
Siku ya Jumatatu, msanii Wazo Baba ndio alikua ameachia wimbo wake wa LINDA aliomshirikisha Susumila , pia ndio siku ambayo walikua wana,shoot video ya wimbo huo. Wakiendelea ku,shoot video hio, ilifika katika scene moja ambayo wasanii hao wawili walikua waingize ni kama wanapigania mwanamke. Katika ku,shoot scene hio, Wazo Baba kwa bahati mbaya alim,wahi Susumila ngumi ya ukweli, kwa uchungu aliouskia naye Susumila akalipiza kimaksudi ngumi ya ukweli kwa Wazo Baba . Stori ikabadilika sasa, scene ya kuigiza kwa video ikawa ndio uwanja wa ndondi. Ilibidi waliokuwepo waingilie kati kuwatenganisha lakini tayari wawili hao walikua wametoana damu. Walipotenganishwa tu, Susumila alifululiza hadi alipokua ameegesha dereva wake na kumwambia waondoke. Juhudi za watu kujaribu kumtuliza Susumila na kumuomba asiondoke katika shoot hio ziliambulia patupu na kupelekea kukatishwa kwa utayarishaji wa video. 'Ilikua bahati mbaya tu. Katika ile hali ya kuigiza,  kuvutana nkajisahau n...

Serah Sarah Afanya Makubwa Na Producer Wa 'Selfie' Ya Koffi Olomide Nchini Rwanda

Image
Mastola  ni producer gwiji katika eneo la Afrika Ya Kati, ambaye ni mzaliwa wa Rwanda. Nchini Rwanda na Congo, yeye ni mmoja kati ya ma,producer ambao wameshikilia sanaa ya mziki, hio ni kutoka kwa ujuzi wake mkubwa ambao umemfanya afanye kazi na wasanii tajika kama vile Koffi Olomide, Cool Matope, Fally Ipupa, marehemu Papa Wemba na wengine wengi. Msanii kutoka Mombasa, hitmaker wa Cheza Kidogo, Serah Sarah alifunga safari hadi nchini Rwanda ili kumfuata producer huyu ambaye walikua wamefahamiana alipokua akiishi Dubai. Walipatana na wakiwa pamoja na Guitarist gwiji, Ibrahim Tamfum , wakafanya PAPASA,  ( IKO HAPA ) ambayo waliirekodia katika studio ya Matola Music na kufanya video kabisa ya wimbo huo....itazame hapa chini...

Dazlah Aongelea Kuhusu Tuhuma Za Ku,copy Wimbo Wa Chege Na CDiamond Platnumz

Image
Msanii Dazlah amefunguka na kuwahakikishia mashabiki wake kuwa bado yuko imara na wanafaa kutarajia mengi kutoka kwake. Hii ni baada ya mmoja ya mashabiki wake kumuuliza kwa nini hatoi hits mfano wa Kidekide iliyofanya vizuri sana. Kulingana na Dazlah ni kwamba tangu atoe Kidekide ametoa hits nyingi sana lakini kwa vile Kidekide bado haijaisha mtaani, imekua vigumu sana kwa mashabiki kuzikubali track hizo. Vilevile, Dazlah amedai ya kwamba yeye hurekodi kila siku na kapuni ana nyimbo zaidi ya mia mbili ambazo hajaziachia bado. "Tangu nitoe Kidekide sijakaa serious nikasema eti nafanya ngoma kwa maana nilikua nashughulikia mambo flani kuweka ma,dancers wangu sawa, kutengeneza ofisi yangu na Chilemonde , kwa hivyo sikutaka kukaa kimya ndio maana nikatoa ngoma kadhaa hapa katikati kama vile Nitalia na Ringa " . Je anazizungumziaje tuhuma za kukopi wimbo wa Diamond Platinumz na Chege-Waache Waoane kwenye ngoma yake ya Waache Waongee ? Msikilize Dazlah akifunguka...

Dogo Richy Na Shyman Warushiana Maneno Mazito Kuhusu Beef Yao.

Image
  Mapema mwaka huu, hitmaker wa Yoyoba, Dogo Richy alianzisha label yake, RICLAM ENTERTAINMENT ambaye alisema ya kwamba ameianzishwa kwa nia ya kukuza wasanii ambao wana kipaji ila hawajaweza kutoka na wasanii alioanza kuwa,sign walikua Batengo na Shyman. Lakini baadaye label hio ilionekana ni kama imekufa vile, kwa sababu hakuna kilichokua kinaskika kutoka kambi hio. Baadae ilisemekana ya kwamba Batengo na Shyman walikua wametimuliwa kutoka label hio, kisa? Kulingana na Dogo Richy, ni kwamba wawili hao walipata umaarufu kidogo na wakaanza kuvimba kichwa, haswaa Shyman alipopata airplay kidogo baada ya kuachia wimbo wa TULIA ambao kulingana na Richy, yeye ndio aliutunga wimbo huo na Shyman aliuachia hata bila idhini yake. Dogo Richy amefunguka mengi mazito kuhusu kutibuana kwake na Shyman   >> HAPA Kwa upande wake naye Shyman amefunguka na kusema ya kukana madai ya yeye kuvimba kichwwa na kukataa kua wimbo huo ulitungwa na Dogo Richy. Kulingana na Sh...

Mmoja Wa Wasanii Wenye Bidii Zaidi Kutoka Pwani

Image
Ukiweka kando kidogo wasanii ambao tayari wamejipa majina, kuna wasanii ambao ndio wanakua. Hilo ndio kundi ambalo la wasanii ambao wanahitaji nguvu sana ilikupenya kwa sababu waliotangulia tayari washajitengenezea soko na haiwachukui nguvu nyingi kuskuma kazi zao tofauti na hawa ambao ndio bado wanajaribu kutengeneza connections mbili tatu na kujifunza vitu kadhaa katika sanaa na biashara ya mziki.   Kati ya fungu hilo la wasanii, Mombasa kuna msanii Romromy ambaye anaonyesha kukua kwa kasi kwani ana bidii ya mchwa. Baada ya kutoa track yake ya kwanza ya 'Hapa Kenya ' na baadae ' Ujaluo Utaniua' , Romromy ameamua hatapumzika kwani tayari ameachia video yake mpya ya ' End Month '  ambayo audio yake imeatayarishwa na Naiboi/Pacho Entertainment. Kwa mwendo huu na kujitahidi kufanya kazi ni ishara tosha ya kwamba Romromy ni mmoja ya wasanii ambao ni wakuangalia na kutarajia vitu vikubwa sana mwaka wa 2017... Hii hapa ni video yake mpya..